Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Vikosi vya Ukraine vimemkamata mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyetumwa kusaidia jeshi la Urusi, zimearifu taarifa za kijasusi za Korea Kusini siku ya Ijumaa, Desemba 27.

Hiki ni kisa cha kwanza kujulikana cha Mkorea Kaskazini aliyekamatwa akiwa hai tangu Kyiv na nchi za Magharibi ziripoti kuwa Pyongyang ilituma wanajeshi kumuunga mkono mshirika wake, Urusi.
“Kama sehemu ya upashanaji habari wa wakati halisi na idara ya ujasusi ya nchi washirika, imethibitishwa kuwa mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyejeruhiwa amekamatwa,” idara ya ujasusi ya Korea Kusini imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari, bila maelezo zaidi juu ya mazingira ya kukamatwa kwa askari huyo.
Uthibitisho huo unakuja baada ya picha inayodaiwa kumuonyesha askari aliyejeruhiwa kusambaa kwenye Telegram.
Korea Kaskazini imetuma zaidi ya wanajeshi 10,000 kuisaidia Urusi, kulingana na Kyiv na Seoul – ingawa Moscow na Pyongyang hazijathibitisha wala kukanusha kuwepo kwao.
Wanajeshi 12,000 wa Korea Kaskazini wako kwenye uwanja wa vita?
Kulingana na Kyiv, wanajeshi 12,000 wa Korea Kaskazini, wakiwemo “maafisa 500 na majenerali watatu”, wako katika jimbo la Urusi la Kursk, ambalo jeshi la Ukraine limechukua mamia ya kilomita za mraba tangu mwezi Agosti.
Urusi wala Korea Kaskazini hazijawahi kuthibitisha kuwepo kwa kikosi hiki kusaidi jeshi la Urusi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alihakikisha Jumatatu kwamba karibu wanajeshi 3,000 wa Korea Kaskazini “wameuawa au kujeruhiwa” tangu kushirikiana na jeshi la Urusi katika vita vya Ukraine. Seoul kwa upande wake ilitaja siku ya Jumatatu watu 1,100 “waliouawa au kujeruhiwa”
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.