Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Zaidi ya wahamiaji 10,400 walifariki au kutoweka baharini walipokuwa wakijaribu kuingia Uhispania mnamo mwaka 2024. Njia mbaya zaidi ulimwenguni ni njia ya Atlantiki inayounganisha Senegal, Mauritania au Morocco hadi Visiwa vya Canary. Inachukua karibu 95% ya wahanga wa mwaka huu, kulingana na ripoti iliyochapishwa siku ya Alhamisi, Desemba 26 na shirika lisilo la kiserikali la Uhispania la Caminando Fronteras.
Zaidi ya wanawake 400 na watoto 1,500 walifariki wakitumia nji hii kwa usafiri wa majini kuelekea Uhispani. Takwimu zisizo za kawaida zinazofanya 2024 kuwa mwaka mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa.
Njia pekee ya Mauritania hadi Canary ilisababisha vifo vingi zaidi ya njia zote walizotumia wahamiaji mwaka jana. Kwenye boti zilizokumbwa na aajali hizi, walipatkana hasa watu kutoka Sahel, wanaokimbia vita pamoja na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa na vurugu za eneo lenye uhasama.
Mwaka huu 2024, kulikuwa na karibu vifo 30 kwa siku, kati ya mwezi wa Januari na Desemba 15, kwenye njia tofauti za uhamiaji kwenda Uhispania, au waathiriwa 10,400 kwa jumla. Watu hawa walitoka angalau nchi 28, haswa Afrika Magharibi, lakini pia Pakistan na Yemen. Idadi ya vifo ni 58% zaidi ya ile iliyorekodiwa na shirika lisilo la kiserikali la Uhispania la Caminando Fronteras mwaka jana; lilirekodi wahamiaji 6,618 waliofariki au kutoweka wakati wahamiaji wakijaribu kwenda Uhispania mnamo mwaka 2023.
Idadi ya vifo baharini imeongezeka maradufu katika mwaka mmoja
Kulingana na shirika hili lisilo la kiserikali, ikiwa idadi ya vifo imeongezeka karibu mara mbili mwaka huu, ni kwa sababu ya kupuuzwa kwa jukumu la uokoaji. Takwimu ambazo kwa hivyo zinaonyesha kitendo: nchi hutanguliza udhibiti wa uhamiaji juu ya haki ya kuishi. Shirika hili pia linashtumu matumizi ya boti hatari, kuondoka katika hali mbaya ya hali ya hewa, ukosefu wa chakula na hata vifaa vya urambazaji.
Safari kutoka Mauritania hadi Canary hazikukoma, hata wakati hali ya hewa ilikuwa ngumu sana. Kuzama kwa meli mara kwa mara hakukatishi tamaa wasafirishaji, haswa kwa kuwa njia hii haifuatiliwi sana kuliko zingine.
Idadi ya wahamiaji haramu pia imeongezeka
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uhispania, waliofanikiwa kuingia Uhispania kinyume cha sheria mnamo 2024, kwa njia ya ardhini au baharini, ni zaidi ya 60,000, pamoja na 43,737 waliofika kwenye visiwa vya Canary kati ya mwezi Januari na katikati ya mwezi Desemba, ikilinganishwa na 36,888 kwa jumla mwaka jana, ongezeko la 18.6%. Ujio huu mkubwa umesukuma mamlaka ya Visiwa vya Canary kupiga kelele, ikisema haswa kwamba hawana uwezo wa kudhibiti mmiminiko wa watoto wadogo ambao ni lazima wawatunze katika vituo vya mapokezi.
Kati ya mwaka 2014 na 2024, zaidi ya wahamiaji 16,400 walifariki au kutoweka barani Afrika, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM). Kielelezo ambacho kinajumuisha vifo wakati wa kuvuka kuelekea Canary, lakini pia wale walio katika Jangwa la Sahara.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.