Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Israel imefanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo kadhaa yanayohusiana na Wahuthi nchini Yemen, yakiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sanaa na bandari za Bahari ya Shamu, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua sita na kuwajeruhi kadhaa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Wahuthi na Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi hayo, ambayo pia yamelenga vituo vya umeme na miundombinu ya kijeshi, yalifuata mashambulizi ya makombora na droni ya Wahuthi dhidi ya Israel, yaliyotajwa kama ishara ya mshikamano na Wapalestina.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na wafanyakazi wengine wa Umoja wa Mataifa walikuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Yemen mjini Sanaa siku ya Alhamisi wakati wa shambulizi la anga la Israel.
Katika chapisho la mtandao wa kijamii, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema yeye na wafanyikazi walikuwa karibu kupanda ndege wakati uwanja wa ndege ulipopigwa na angani.
“Mmoja wa wafanyakazi wa ndege yetu alijeruhiwa,” aliandika, akiongeza kuwa watu wawili katika uwanja wa ndege waliuawa.
Mashambulizi hayo – ambayo pia yamegonga vituo vya umeme na bandari – yamesababisha vifo vya watu wasiopungua watatu huku zaidi ya dazeni wakijeruhiwa, kulingana na vyombo vya habari vinavyoendeshwa na Houthi.
Wahuthi, ambao ni sehemu ya muungano wa Iran unaojulikana kama “mhimili wa upinzani,” walitishia kujibu, hali inayochochea mvutano zaidi katika kanda hiyo.
Umoja wa Mataifa umelaani mzozo huo, ukionya kuwa mashambulizi kwenye miundombinu ya Yemen yanahatarisha misaada ya kibinadamu, ambayo inategemewa na karibu asilimia 80 ya Wayemeni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amelaani ongezeko la makabiliano kati ya Israel na waasi wa Kihuthi nchini Yemen, ambayo Umoja wa Mataifa unasema yanatishia kuzidisha mzozo Mashariki ya Kati.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.