Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Maandamano yameshuhudiwa nchini Syria, kulaani kitendo cha kuteketezwa moto kwa mti maalum wa kuashirikia sikukuu ya Krismasi, wakati huu uongozi mpya nchini humo ukishinikizwa kulinda haki za dini zote.
Mkanda wa video uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii, imewaonesha wanaume waliokuwa na silaha wakitekeza moto mti huo wa Krismasi katikati ya nchi hiyo, eneo ambalo kuna idadi kubwa ya Wakiristo.
Kitendo hicho kimezua maandamano, huku uongozi wa chama cha Kiislamu cha Hayat Tahrir al-Sham (HTS), kikisema kuwa wapiganaji wa kigeni waliohusika wamekamatwa.
Hili limekuja baada ya uongozi huo mpya, ulioangusha utawala mrefu wa Bashar Al Assad kutangaza na kuahidi kuwalinda watu wote wanaoishi nchini Syria wakiwemo waumini wa dini, zisizo na watu wengine kama Wakiritso.
Katika hatua nyingine, uongozi hup mpya wa Syria umesema kuwa umeingia kwenye makubaliano na makundi ya waasi yenye silaha, ambayo yamekubali kuunda jeshi moja nchini humo.
Nch ya Qatar nayo imesema baada ya kuondolewa madarakani kwa Assad, jumuiya ya Kimataia inapaswa kuondoa haraka vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo baaada ya kuzuka kwa vita dhidi ya utawala wa wakati huo mwaka 2011
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.