Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wananchi wa Chad wanajiandaa kupiga kura siku ya Jumapili katika uchaguzi wa wabunge na viongozi wa serikali za mitaa, ambao vyama vya upinzani unasema huatakuwa huru na haki na kuamua kuususia.

Kiongozi wa Chad anatarajiwa kutumia uchaguzi huo, kuimarisha nafasi yake kama rais wa nchi hiyo, baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwaka 2021 kufuatia kifo cha baba yake, Idris Deby aliyeuawa katika mapambano na waasi. © FMM RFI Studio graphique
Kuelekea uchaguzi huo, rais Mahamat Idriss Deby Itno amesema, uchaguzi huo ni hatua muhimu ya kuelekea katika mabadiliko ya kidemokrasia katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Kiongozi huyo anatarajiwa kutumia uchaguzi huo, kuimarisha nafasi yake kama rais wa nchi hiyo, baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwaka 2021 kufuatia kifo cha baba yake, Idris Deby aliyeuawa katika mapambano na waasi.
Wachambuzi wa siasa nchini Chad, wanasema Mahamat atatumia uchaguzi huo kuoneshe kuwa anakuza demokrasia katika nchi yake, lakini kwa upande mwingine, huenda uchaguzi huo ukazua athari kubwa kisiasa kwa mustakabali wa taifa hilo baada ya upinzani kususia.
Uchaguzi huo unafanyika wakati huu taifa La Chad likikumbwa na changamoto za usalama katika ukanda wa Ziwa Chad kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara yanayozababishwa na kundi la Boko Haram na makundi mengine ya kijihadi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.