Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mitaa ya Bethlehem, katika Ukingo wa Magharibi, ilikuwa kimya siku ya Jumanne jioni ya Krismasi, bila mti wa Krismasi au mapambo, kwa mshikamano na Wakristo wa Gaza. Misa ya usiku wa manane imeadhimishwa katika Kanisa la Nativity, ambapo kulingana na imani, Kristo alizaliwa, lakini waumini hawakuwa na moyo wa kusherehekea

Licha ya nyimbo mbalimbali, hali ilikuwa nzito katika kanisa ya Nativity huko Bethlehemu. Katika mahubiri yake, kiongozi wa kanisa la Jerusalem, Pierbatista Pizzaballa, ametoa pongezi kwa Wakristo wa eneo la Palestina: “Nina wazo kwa ajili ya ndugu zetu wa Gaza, na ninarudia maombi yetu ya ukaribu na mshikamano kwao. Hamko peke yenu.”
Kwenye madawati, nyuso za wawakilishi wa mamlaka ya Palestina zimeonyesha masikitiko yao, waumini wengi walikuwa na huzuni. “Hakuna taa, hakuna mti wa Krismasi, hakuna nyuso za furaha … hata hisia za watu zimepungua,” anaelezea mwanamke mmoja.
Alexis Janson, 36, ni mmoja wa mahujaji wachache waliokuja kutoka nje ya nchi Jumanne jioni. Aliwasili kwa mguu kutoka Tours katika muda wa miezi sita. “Mambo yanayotokea leo ni ya kutisha kwa roho hizi zote zinazoteseka, familia hizi zote ambazo zimesambaratika, tunapaswa kuomba ili hali iweze kuimarika na watu wapate amani,” anabainisha HAlexis Janson.
Tamer ni Mkristo wa Kipalestina, kama wengine wengi, hana furaha yoyote kwa siku ya leo ya Krismasi: “Inasikitisha, inasikitisha sana… Tangu kuanza kwa vita huko Gaza, huzuni imeenea. Unahisi mvutano huu, huzuni huu. “
Wakristo wengi waliohudhuria mis Jumatanu jioni wametoa wito wa kusitihwa kwa mapigano na kusema hawatafurahia Krismasi ya tatu nyakati za vita.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.