DRC: Jeshi la FARDC na wanamgambo wa M23 wanapambana eneo la Mambasa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tangu mwishoni mwa juma lililopita kumeendelea kuripotiwa mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali wanaosaidiwa na wapiganaji Wazalendo dhidi ya waasi wa M23 wanaosaidiwa na nchi ya Rwanda.

Wanajeshi wa FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) wakati wa operesheni dhidi ya waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) huko Opira, Kivu Kaskazini, Januari 25, 2018.
Wanajeshi wa FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) wakati wa operesheni dhidi ya waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) huko Opira, Kivu Kaskazini, Januari 25, 2018. © AFP

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, mapigano yaliripotiwa kwenye eneo la Lubero lililoko umbali wa kilometa 150 kaskazini mwa mji wa Goma.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha mwaka mmoja, jeshi lilitumia helikopta za kivita kuwakabili waasi wa M23, ikiwa ni katika juhudi za kuzidisha udhibiti wao hadi mji wa Alimbongo baada ya kufanikiwa kuteka eneo la Mambasa na Kanyabi.

Serikali ya DRC na washirika wake imekuwa ikipambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC.
Serikali ya DRC na washirika wake imekuwa ikipambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC. AFP – GLODY MURHABAZI

Makabiliano yameongezeka zaidi tangu kutangazwa kuvunjika kwa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yanaratibiwa na Serikali ya Angola.

Mashirika ya kiraia wilayani Lubero yanasema mapigano haya yamesababisha wimbi jipya la wakimbizi wanaokimbia makazi yao.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment