Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria hivi punde siku ya Jumamosi Desemba 21, 2024 imekanusha katika taarifa kwa vyombo vya habari shutuma zilizotolewa na Niger, ambayo iliishutumu kwa kutaka “kuhatarisa usalama wake”.
Nchi hiyo ilishutumu Nigeria kwa “kutumikia kama msingi wa nyuma wa kuvuruga utulivu wa Niger” kwa kushirikiana na baadhi ya mataifa ya kigeni na vigogo wa utawala wa zamani nchini humo. Baada ya kumwita mwakilishi wa ubalozi wa Nigeria huko Niamey, Nigeria iliishia kukataa shutuma hizi katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Serikali ya Nigeria imesema “ina wasiwasi sana” na ikathibitisha “kwa uthabiti kwamba hakuna wanajeshi wa Ufaransa kaskazini mwa nchi wanaojiandaa kuivuruga serikali ya Niger.” Msemaji wa wizara hiyo ameongeza kuwa “madai haya hayana msingi na yanapaswa kufutiliwa mbali kabisa.”
Mzozo huo ulianza mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger aliposoma taarifa kwa vyombo vya habari kwenye televisheni ya taifa; ambapo aliishutumu Nigeria kwa kutaka “kuhatarisha usalama” wa nchi pamoja na kushiriki katika njama kwa msaada wa mataifa ya kigeni.
Mvutano huu unakuja wakati bomba, ambalo husafirisha mafuta ya Niger hadi Benin kwenye mpaka wa Nigeria, limeharibiwa mara tatu katika muda wa chini ya wiki mbili na watu wenye silaha ambao Niamey inawatuhumu kutoka Nigeria. Shutuma pia zilikanushwa katika taarifa ya vyombo vya habari vya Nigeria, ambayo inazingatia kwamba shambulio hili lilitekelezwa na “kundi la kigaidi la Lakurawa”.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulidorora kufuatia mapinduzi ya mwaka 2023, kuundwa kwa AES na kutangazwa kwa kuondoka kwake kutoka ECOWAS.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.