Msumbiji: Raia wanasubiri kwa hamu kujua uamuzi kuhusu matokeo ya uchaguzi ambao ulizozaniwa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Raia wa Msumbiji hivi leo wanatarajiwa kufahamu hatma ya matokeo ya uchaguzi wa mwezi Octoba uliogubikwa na utata, kufuatia madai ya wizi wa kura na udanganyifu, matokeo yaliyosababisha maandamano ya upinzani nchi nzima ambapo watu kadhaa wameuawa kutokana na vurugu hizo.

Contagem dos votos numa mesa de voto em Maputo, Moçambique. 9 de Outubro de 2024.
Maafisa wa uchaguzi wahesabu kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Msumbiji katika kituo cha kupigia kura mjini Maputo, Msumbiji, tarehe 09 Oktoba 2024. © LUSA – José Coelho

Hatma ya matokeo hayo ambayo yalikipa ushindi chama tawala cha Frelimo, sasa iko mikononi mwa baraza la kikatiba ambalo litaamua ikiwa lithibitishe matokeo hayo au la.

Kinara wa upinzani Venancio Mondlane, ametishia kuitisha maandamano zaidi ikiwa baraza la kikatiba litaamua kuthibitisha matokeo hayo, ambapo mgombea wa chama tawala Daniel Chapo alipata asilimia 70 ya kura zote akifuatiwa na Mondlane aliyeambulia asilimia 20.

Mgombea Urais na Katibu Mkuu wa Frelimo Daniel Chapo akipiga kura katika kituo cha kupigia kura huko Inhambane, Msumbiji, 09 Oktoba 2024.
Mgombea Urais na Katibu Mkuu wa Frelimo Daniel Chapo akipiga kura katika kituo cha kupigia kura huko Inhambane, Msumbiji, 09 Oktoba 2024. LUSA – CRESPO CUAMBA

Kwa wiki kadhaa sasa taifa hilo limeshuhudia vurugu za kisiasa na hata wapinzani kadhaa kuuawa, katika uchaguzi ambao hata viongozi wa kidini, waangalizi wa ndani na nje walisema uchaguzi ulikuwa na dosari ikiwemo baadhi ya matokeo kubadilishwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment