Unataka Kustaafu Ukiwa Na Uhuru Wa Kipato?…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Awamu 4 Kubwa Utakazopitia Baada Ya Kustaafu

i. Kuwa Likizo
ii. Kupoteza Na Kupotea
iii. Kujaribu Vitu Vipya
iv. Kutengeneza Mwanzo Mpya

Katika makala hii tutazungumzia awamu ya kwanza.

– Kuwa Likizo

Mara baada ya kutoka kazini, mstaafu hukutana na kipindi hiki cha kwanza ambacho mara nyingi hudumu kwa muda kama wamwakammojahivi.

Katika kipindi hiki, mstaafu mara nyingi huwa na furaha kwa sababu anakuwa hana misukosuko na watu wengi wanakuwa wanamthamini kwa sababu walimmisi kwa muda mrefu sana kwa sababu kwa miaka mingi alikuwa bize mno.

Baadhi ya vitu ambavyo vinatokea ni pamoja na:

Ideal Retirement (Kufurahia Hali Ya Kustaafu).

Katika kipindi hiki, mstaafu ndio anaona haswa amestaafu kwa sababu anakuwa hana kitu cha kufanya.

Yaani hakuna tena kukimbizana asubuhi kuamka mapema, wala kupigiwa simu na kuuliziwa kuhusu jambo fulani au kuambiwa akafuatilie jambo fulani.

Mara nyingi kwenye kipindi hiki, mstaafu atakuwa anaonyesha kufurahia maisha mapya ambayo hakuwahi kuwa nayo kwa mudamrefu sana.

Kwenye kipindi hiki, utatembelewa na watu wengi sana na kila utakakoenda kutembelea watakupokea kwa furaha sana.

Unakuwa mtu muhimu kwenye jamii yako.

Ila usisahau, huwa hakidumu, utaona kinachotokea kwenye awamu ya pili.

Usipojua namna sahihi ya Kujipanga Kabla Ya Kustaafu, Unaweza jikuta unakuwa na uzee mbaya na magomvi yasiyoisha na watoto kuwa hawakujali.

Kama unataka kujifunza Jinsi ya Kujipanga Vyema Ili Ustaafu Ukiwa Na Uhuru Wa Kipato Na Uzee Mwema LEO nashauri usome eBook yangu ya “KABLA YA KUSTAAFU, Mambo Ya Kuzingatia Ili Uwe Na Maisha Ya Furaha Baada Ya Kustaafu”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment