Urusi yaanza kuondoa meli zake za Mediterania nchini Syria

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mara tu utawala wa Bashar Al Assad ulipoanguka, Kremlin ilionyesha kwamba ilikuwa inawasiliana na mamlaka mpya ya Syria kuhusu vituo vyake viwili: kambi ya wanamaji ya Tartus na kambi ya anga ya Hmeimim, karibu na Latakia.

Wanajeshi wa Urusi walioko Syria walifanya mazoezi makubwa mnamo mnamo mwezi wa Septemba. Hapa ilikuwa Septemba 12, 2024, karibu na Tartus.
Wanajeshi wa Urusi walioko Syria walifanya mazoezi makubwa mnamo mnamo mwezi wa Septemba. Hapa ilikuwa Septemba 12, 2024, karibu na Tartus. © Service de presse du ministère russe de la Défense / via AP

Lakini wakati Moscow, pamoja na Tehran, walikuwa washirika wakuu wa kijeshi wa utawala ulioanguka wa Assad, nafasi ya kufikia makubaliano inaonekana kuwa ndogo. Kipindi cha kukosekana kwa utulivu kinaanza na Jeshi la Wanamaji la Urusi linamua kujiondoa kabisa kaika ardhi ya Syria.

Kuanguka kwa utawala wa Bashar Al Assad pia kulishangaza Urusi. Kwa miezi kadhaa tayari, Moscow ilikuwa imejiondoa hata kwa hatua kutoka Syria, ikipendelea kuendeleza na vita vyake nchini Ukraine. Kamandi ya kambi za Urusi ilichukuliwa na maafisa ambao walionekana kuwa hawana nguvu katika vita  vya Ukraine, kulingana na duru za kuaminika. kamandi hii kwa hakika ilishindwa kutathmini kwa usahihi tishio la waasi wa Kiislamu.

Kuanzia siku za kwanza za uasi na baada ya kufanya mashambulizi machache na yasiyofaa dhidi ya waasi wa Kiislamu, Moscow ilijipanga haraka ili kuzuia zana zake za kijeshi na silaha zisianguke mikononi mwa Hayat Tahrir al-Sham ( HTS). Kundi hili ndilo linaloongoza muungano wa waasi unaotawala sasa Damascus. Baada ya kuweka vifaa vyake vingi vya kimkakati huko Tartus, jeshi la Urusi liliamua kuhamisha silaha hizo kwa ndege za usafiri kutoka kituo cha anga cha Hmeimim, kilichoko Latakia.

Kuanzia sasa, Moscow inaonekana kuanza zoezi la uhamishaji kamili zana zake zote kutoka kambi zake zote mbili na haswa kituo chake cha jeshi la majini huko Tartus. Baada ya kushiriki katika zoezi kubwa la urushaji makombora katika Mediterania ya Mashariki, meli kubwa ya Gorshkov iliondoka kwenye Mediterania baada ya miezi minane ya misheni. Hii ikiambatana na meli ya kijeshi ya Yelnya. Gorshkov iliondoka Tartus mnamo Desemba 5, na hakurudi nyuma kusaidia serikali ya Syria au kulinda miundombinu ya Urusi.

Kisha meli za jeshi la wanamaji – angalau meli tatu kubwa na manowari – zilisafiri mnamo Desemba 8, labda kama sehemu ya hatua ya ulinzi. Inawezekana kwamba Moscow ilijua juu ya mashambulio ya Israeli ambayo yaliharibu meli za Syria huko Tartus mnamo Desemba 9 na 10.

Meli za kivita zinaondoka, meli za mizigo zinawasili

Mnamo Desemba 8, meli ya kivita ilipoondoka kwenye bandari ya Tartus, meli za uchukuzi za Shabalin, Ostrakovskiy na Gren, na vile vile meli ya msaada ya Churov, ziliondoka katika bandari zao za katika Bahari ya Baltic na Kaskazini kuelekea Bahari ya Mediterania. Mwendo wa kuondoka kwao unaweza kuashiria kwamba walikuwa wamekesha kwa siku kadhaa.

Kufikia Desemba 10, walikuwa bado wanavuka kuelekea Mediterania. Chaguo mbili zinapatikana kwa Moscow: ama meli hizi za usafiri zinapanga kurejesha vifaa nchini Urusi, au zitatafuta kutegemea bandari nyingine katika Mediterania. 

Tobruk nchini Libya inaweza kuwa enro lingine la msaada. Operesheni kama hiyo ilifanywa mnamo mwez Machi na Aprili 2024 na LST Ostrakovskiy na Gren, zikisindikizwa na mreli kubwa iitwayo Merkuriy, kati ya Tartous na Tobruk.

Vifaa vya meli ya msaada ya Churov vinaweza, kwa upande wake, kuwa na lengo la kusindikiza manowari ya SSK Novorossiysk kwa kurudi kwa kikosi cha wanamaji kinachopiga kambi huko Kaskazini.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment