Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Waokoaji wanaendelea siku ya Jumatano, Disemba 18 kuwatafuta manusura katika vifusi vya majengo yaliyoharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi lililopiga mji mkuu wa Vanuatu na kusababisha vifo vya takriban watu 14, kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.3 kwenye vipimo vya Richter, lilitokea saa 6:47 mchana kwa saa za huko siku moja kabla kwenye kisiwa kikuu cha visiwa vya Pasifiki, ambapo Port Vila inapatikana. Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu katika Pasifiki, Katie Greenwood, ametangaza idadi ya “vifo 14 vilivyothibitishwa na majeruhi 200 wanaotibiwa katika hospitali kuu ya Port Vila”, akinukuu serikali ya eneo hilo.
“Miundombinu ya hospitali imeharibiwa (…) nyumba nyingi zimeharibiwa,” ameandika, akiongeza kuwa “hifadhi ya maji” pia imeathirika.
Majengo kadhaa yameporomoka, likiwemo lile laubalozi wa Ufaransa, “lililoharibiwa” kulingana na balozi wa nchi hiyo, na kubainisha kuwa wafanyakazi wa kidiplomasia wako “salama salimini”.
Msaada wa kimataifa
Matetemeko ya ardhi hutokea mara kwa mara huko Vanuatu, visiwa vya mwinuko wa chini vya wakaazi 320,000 vilivyo kwenye Gonga la Moto la Pasifiki, safu ya shughuli kali ya tectonic ambayo inaenea juu ya sehemu kubwa ya ukingo wa bahari hii.
Imeorodheshwa miongoni mwa nchi zilizo hatarini zaidi kwa majanga ya asili kama vile matetemeko ya ardhi, dhoruba, mafuriko na tsunami, kulingana na Ripoti ya Kila mwaka ya Hatari ya Dunia.
Ufaransa inasimama “pamoja na mamlaka ya Vanuatu” na iko tayari “kuchangia shughuli za misaada” ikiwa itaomba, Wizara yake ya Mambo ya Nje imetangaza Jumanne.
New Zealand, kwa upande wake, imetuma ndege ya uchunguzi ili kutathmini uharibifu, Waziri wa Mambo ya Nje Winston Peters amesema katika taarifa yake, akipendekeza kutuma wafanyakazi na vifaa “mara tu uwanja wa ndege wa Port -Vila utakapofunguliwa tena.”
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.