Makumi ya watu hawajulikani walipo baada ya ajali ya boti nchini DRC

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Boti iliyokuwa imejaza mizigo ilipinduka kwenye mto katikati mwa DRC siku ya Jumanne, na kuua takriban watu 25, wakiwemo watoto, na makumi ya watu hawajulikani waliko, maafisa na wakaazi wa eneo hilo wamesema.

Takriban watu 78 walikufa maji mwezi Oktoba wakati boti iliyokuwa imejaa mizigo ilipozama mashariki mwa nchi hiyo, huku 80 wakipoteza maisha katika ajali inayofanana na hiyo karibu na Kinshasa mwezi Juni.
Takriban watu 78 walikufa maji mwezi Oktoba wakati boti iliyokuwa imejaa mizigo ilipozama mashariki mwa nchi hiyo, huku 80 wakipoteza maisha katika ajali inayofanana na hiyo karibu na Kinshasa mwezi Juni. AFP – ARSENE MPIANA

Inaripotiwa kuwa boti hiyo ilikuwa na zaidi ya abiria 100 baada ya kuondoka katika mji wa Inongo, kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kinshasa. Ilipinduka mita mia chache baada ya safari yake kwenye Mto Fimi, mkasa wa hivi punde zaidi wa aina yake kuikumba DRC.

Shughuli ya kuwatafuta waliotoweka ilikuwa ikiendelea saa chache baadaye siku ya Jumanne huku kukiwa na hofu kuwa idadi ya waliofariki ni kubwa zaidi.

“Boti ilikuwa imebebea mzigo mkubwa kwenye kiwango cha paa na kuhusu maiti, angalau 25 zimepatikana hadi sasa,” David Kalemba, kamishna wa mto Inongo amesema.

Boti hiyo iliyopinduka pia ilipakiwa na bidhaa, kulingana na Alex Mbumba, mkazi wa eneo hilo. “Miongoni mwa waliofariki ni watoto, lakini ni vigumu kutoa idadi kamili kwa sasa kwa sababu (…) boti ilikuwa na abiria wengi,” amesema Bw. Mbumba akinukuliwa na shirika la Associated Press.

Ajali hiyo ya Jumanne ni ya nne mwaka huu katika mkoa wa Maï-Ndombe, eneo ambalo limezungukwa na mito na ambapo wengi wanategemea usafiri wa mtoni.

Mamlaka ya Kongo mara nyingi imeonya dhidi ya upakiaji kupita kiasi na kuahidi kuwaadhibu wale ambao hawaheshimu hatua za usalama za usafiri wa mtoni. Hata hivyo, katika maeneo ya mbali ambako abiria wengi wanatoka, wengi hawawezi kumudu usafiri wa umma kutokana na barabara chache zilizopo.

Takriban watu 78 walikufa maji mwezi Oktoba wakati boti iliyokuwa imejaa mizigo ilipozama mashariki mwa nchi hiyo, huku 80 wakipoteza maisha katika ajali inayofanana na hiyo karibu na Kinshasa mwezi Juni.

“Serikali lazima ichukue hatua kuboresha usalama kwenye maji ya mkoa  wetu (kwa sababu) hali ya usafiri mtoni  ni hatari,” ameongeza Bw. Mbumba.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment