Chuma Hunoa Chuma-17-12-2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Fundi mmoja alipewa na tajiri kazi ya kupaka mtumbwi rangi.
Wakati anapaka rangi akagundua kuwa kwenye ule mtumbwi kuna sehemu ndogo kwa chini imetoboka.

Fundi alichofanya akarekebishe lile tobo na kuendelea na Kazi yake ya kupaka rangi.

Baada ya kumaliza alimwona tajiri akapewa chake na kuondoka.

Tajiri akaingia ndani kupumzika. Vijana wake wakarudi kutoka shule, wakabadilisha nguo na kuchukua mtumbwi kuingia majini kama kawaida kutafuta vitoweo.

Baba yao kushutuka kutoka usingizini, tayari ishakuwa mida ya jioni.

Kaanza kuwaita Vijana wake kama wapo ndani. Hakuna Mtu!!

Akachungulia nje, hakuna Mtumbwi.

Akajaa HOFU na wasiwasi Kwa sababu alijua kabisa ule mtumbwi Una tobo na HAKUMWAMBIA FUNDI ALIZIBE.

Alichoka ghafla. Mara kutazama kwa mbali maeneo ya baharini, akaona Vijana wake, wameegesha mtumbwi pembeni tayari kurudi nyumbani.

Baba aliwakimbilia wanae, Kabla hata hajawasemesha, akaanza kukagua ule mtumbwi.

Hakuamini macho yake, Fundi aliziba lile tobo japo HAKUMWAMBIA….”Fundi alifanya kama Bonus Tu”.

Kesho yake tajiri akamtafuta yule na kumwongezea tena hela.

Fundi akamuuliza kwanini Mzee?

Mzee: Fundi Chukua hiyo ni kwa sababu umeliziba lile tobo Kwa mtumbwi Japo sikukuambia.”

Fundi: Lakini Mzee hiyo Mbona ni kawaida tu, ni sehemu ndogo sana ile, hata haina GHARAMA yoyote Boss.

Tajiri: Fundi hata hiyo haitoshi kwa Wema uliyoonyesha Kwangu Jana. Unajua baada ya Wewe kuondoka nilala, Vijana waliporudi shule wakachukua chombo kwenda baharini. Fikiria usingejiongeza ukaziba lile tundu leo ingekuwaje?

Umejifunza nini kutoka kwa Fundi na Tajiri?

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment