AFRIKA LEO MCHANA-17-12-2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja

Muhtasari

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Mchana ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 17/12/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Jaji akataa hoja ya Trump ya kutaka atupilie mbali kesi aliyopatikana na hatia

dc

Jaji wa mahakama ya New York ameamua kuwa hatia aliyopatikana nayo Donald Trump katika kesi ya kutoa pesa za kutunza siri ni halali, amekataa hoja ya rais mteule kwamba hatia hiyo inapaswa kutupiliwa mbali kutokana na uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani juu ya kinga aliyonayo.

Mwezi Julai, mahakama ya juu ya nchi hiyo iliamua kwamba marais wana kinga dhidi ya mashtaka ya jinai kwa maamuzi rasmi wanayochukua wakiwa madarakani.

Lakini siku ya Jumatatu, Jaji katika jiji la Manhattan jimboni New York, Juan Merchan – ambaye aliongoza kesi ya Trump – aliwaunga mkono waendesha mashitaka, akisema hukumu juu ya makosa 34 ya uhalifu iko kwenye maamuzi ya Trump yasiyo rasmi.

Uamuzi huo wa kutiwa hatia, ikiwa utadumu utamuweka Trump katika historia ya kuwa mhalifu wa kwanza kuhudumu katika Ikulu ya White House.

Katika uamuzi wake wa kurasa 41, Jaji Merchan alikataa hoja za Trump, akisema ushahidi ulioonyeshwa kwenye kesi hii ulihusu “mienendo isiyo rasmi,” aliandika.

Jaji alibainisha kuwa katika uamuzi wa Mahakama ya Juu imegundua kuwa “si kila kitu anachofanya rais ni rasmi,” hata kama kinafanywa kutoka Ikulu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, msemaji wa Trump, Steven Cheung, alikosoa uamuzi huo na kuutaja kuwa “ukiukaji wa moja kwa moja wa uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kinga ya rais.”

Mwezi Mei, jaji wa New York alimpata Trump na hatia ya kughushi rekodi za biashara.

Hatia hiyo ilitokana na jaribio la Trump la kuficha malipo yaliyofanywa na wakili wake wa zamani, Michael Cohen, ambaye mwaka 2016 alimlipa nyota wa filamu za ngono ili asitoboe siri ya kufanya ngono na Trump.

Wanadiplomasia wa Uingereza wakutana na kiongozi wa waasi mjini Damascus

.

Wanadiplomasia wa Uingereza wamefanya mazungumzo na kiongozi wa kundi la waasi la Syria Hayat Tahrir al-Sham (HTS), kufuatia kumwondoa madarakani rais Bashar al-Assad zaidi ya wiki moja iliyopita.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na idara ya operesheni za kijeshi za kundi hilo zilionyesha kiongozi wa HTS Ahmad al-Sharaa – ambaye zamani alijulikana kama Mohammed al-Golani – akikutana na maafisa wakuu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Miongoni mwa waliopigwa picha pamoja naye ni Ann Snow, mwakilishi maalum wa Uingereza kwa Syria.

HTS ilisema wajumbe walijadili “matukio ya hivi punde” nchini Syria.

Al-Sharaa pia alifanya mahojiano na gazeti la Times ambapo alitoa wito kwa nchi za Magharibi kuondoa vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi ya Syria chini ya utawala wa Assad – ikiwa ni pamoja na kutambuliwa kwa HTS kama shirika la kigaidi.

“Wanapaswa kuondoa vikwazo vyote, ambavyo viliwekwa kwa mhusika na mwathiriwa – mhusika hayupo tena kwa sasa. Suala hili haliko kwa ajili ya mazungumzo,” alisema.

Tundu Lissu adai ‘wasiojulikana’ wanapanga njama za kumdhuru

.

Naibu mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA Tundu Lissu amedai kuwa ‘watu wasiojulikana’ wanapanga kumdhuru wakati ambapo chama hicho kinakaribia kufanya uchaguzi wa mwenyekiti.

Katika chapisho lake la mtandao wa X jana usiku, Lissu amesema kwamba ‘watu wasiojulikana’ wanapanga kumdhuru halafu badala yake wamsingizie mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kuwa ndiye aliyetekeleza shambulio dhidi yake.

Amesema kwamba watu hao wamekuwa wakitekeleza mauaji kwa watu wasio na hatia kisha, wanasingizia watu wengine ili waliohusika wasiwajibike na udhalimu walioufanya.

‘’Enyi watu wabaya mjulikanao kama watu wasiojulikana, nimezisikia njama zenu. Mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa chama,’’ ameandika Lissu.

CHADEMA inaelekea kwenye kilele cha uchaguzi wa ndani wa chama hicho huku Lissu akitazamiwa kuchuana na Mbowe kwenye nafasi ya juu zaidi ya chama hicho, na tayari jambo hilo limezua gumzo na hata nyufa baina ya wafuasi wa kambi za Lissu na Mbowe.

‘’Ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe. Ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Septemba 2017 na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed kibao‘’, alisema Tundu Lissu katika chapisho hilo la mtandao wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter.

Mwaka 2017, Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana nje ya makazi yake mjini Dodoma alipokuwa akihudhuria vikao vya Bunge.

Lissu alilizimika kukimbizwa Nairobi, Kenya na baadae Ubelgiji kwa matibabu. Lissu amesalia na ulemavu wa kudumu kutokana na shambulio hilo.

Hakuna mtu aliyekamatwa wala kufunguliwa mashtaka kutokana na shambulio hilo huku Lissu mwenyewe akiilaumu serikali ya utawala wa hayati John Magufuli kwa kutekeleza shambulio hilo, tuhuma ambazo serikali ya Tanzania imezikanusha.

Lissu alisalia ughaibuni baada ya matibabu yake kwa kuhofia usalama wake na alirejea Tanzania mwaka 2020 kugombea urais na Magufuli.

Mara baada ya uchaguzi Lissu alikimbia tena Tanzania huku akitoa shutuma kuwa kuna mipango ya kushambuliwa tena.

Lissu alirejea Tanzania baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani na alisema kuwa amepatiwa hakikisho la usalama wake.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini waliuawa wakipigana na Ukraine – Marekani

.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini wameuawa wakipambana na vikosi vya Ukraine katika eneo la mpaka la Kursk nchini Urusi, Marekani imesema.

Haya yatakuwa majeruhi ya kwanza kuripotiwa tangu ilipojulikana mwezi Oktoba kwamba Korea Kaskazini ilituma takriban wanajeshi 10,000 ili kuimarisha juhudi za vita vya Urusi.

Shirika la kijasusi la kijeshi la Ukraine, GUR, limesema takriban wanajeshi 30 wa Korea Kaskazini wameuawa au kujeruhiwa katika mapigano mwishoni mwa juma.

BBC haijathibitisha madai hayo kwa uhuru.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini – ambao hawana uzoefu wa vita – wanaaminika walitumia wiki zao za kwanza baada ya kutumwa Urusi katika mafunzo na kisha katika majukumu ya usaidizi.

Siku ya Jumamosi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Urusi imeanza kutumia “idadi kubwa” ya wanajeshi hao katika mashambulio yake huko Kursk, sehemu ambayo Ukraine imeiteka tangu ilipoanzisha uvamizi wa ghafla mwezi Agosti.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, katibu wa vyombo vya habari wa Pentagon Meja Jenerali Pat Ryder alisema kuwa Marekani inaamini kwamba wanajeshi wa Korea Kaskazini “wameshiriki katika mapigano huko Kursk pamoja na vikosi vya Urusi” na “wamepata hasara, wote wakiuawa na kujeruhiwa”.

Hakutoa idadi maalum, ingawa alisema wanajeshi hao walikuwa kwenye mapigano tangu “zaidi ya wiki moja iliyopita”.

Jenerali wa Urusi auawa katika mlipuko mjini Moscow

.

Jenerali wa ngazi za juu katika jeshi la Urusi ameuawa katika mlipuko uliotokea mjini Moscow.

Luteni Jenerali Igor Kirillov, mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Nyuklia, Biolojia, Kemikali (NBC), alikuwa akiondoka kwenye makazi yake mapema Jumanne wakati kifaa kilichofichwa kwenye skuta kilipolipulika, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi ilisema.

Iliongeza kuwa msaidizi wa Kirillov pia aliuawa.

Mnamo mwezi Oktoba, Uingereza iliweka vikwazo kwa Kirillov, ikisema alikuwa amesimamia matumizi ya silaha za kemikali nchini Ukraine na alikuwa kiungo muhimu kama “msemaji wa habari za Kremlin”.

Siku ya Jumatatu, idara ya siri ya Ukraine, SBU, ilimfungulia mashtaka bila kuwepo mahakamani, ikisema kwenye Telegram “alihusika na matumizi makubwa ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku”.

Kamati ya Uchunguzi, mamlaka kuu ya uchunguzi ya Urusi, ilisema “imefungua kesi ya jinai ya mauaji ya wanajeshi wawili”.

“Wataalam wa uchunguzi na huduma za uendeshaji wapo katika eneo la tukio,” ilisema.

“Hatua za uchunguzi na shughuli za upekuzi zinafanywa kwa lengo la kubaini hali zote za uhalifu.”

Isabel dos Santos apinga vikwazo vya Uingereza alivyowekewa

.

Tajiri wa Angola Isabel dos Santos, aliyewahi kutajwa kuwa “mwanamke tajiri zaidi barani Afrika”, ameikashifu Uingereza kwa kumuwekea vikwazo, akiambia BBC kuwa hatua hiyo ilishangaza kwani hajapatikana na hatia ya “ufisadi wowote katika mahakama yoyote kwenye nchi yoyote”.

Mwezi uliopita, binti wa rais wa zamani wa Angola alielezewa na serikali ya Uingereza kama “anayetumia mamlaka yake kuiba rasilimali za nchi yao” na mali yake ikashikiliwa na kupigwa marufuku ya kusafiri kwa madai ya kupora mali kutoka kwa nchi ya Angola yenye utajiri wa mafuta.

Alisema serikali ya Angola ilikuwa nyuma ya kampeni ya kumharibia jina.

“Mwisho wa siku hili ni suala la kisiasa,” Dos Santos, 51, aliambia podikasti ya BBC Africa Daily kutoka makao yake huko Dubai.

“Hakukuwa na uchunguzi, ambapo mtu alikuja na kuchunguza na kuangalia ushahidi au kunitaka nifafanue. Hakukuwa na utaratibu,” alisema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy alitangaza vikwazo kwa Dos Santos kama sehemu ya kampeni yake ya kukabiliana na “fedha chafu”.

Taarifa ya serikali ilidai kuwa “ametumia vibaya nafasi zake katika kampuni zinazoendeshwa na serikali kwa ubadhirifu wa angalau £350m [$442m], na kuinyima Angola rasilimali na ufadhili wa miradi ya maendeleo yanayohitajika sana”.

Msemaji wa mwanasheria mkuu wa Angola alisema hawatajadili maelezo yoyote ya kisheria yanayoendelea hadharani lakini akasema kwamba ushahidi wowote wa kuwa nyaraka zilighushiwa zinapaswa kuwasilishwa mahakamani.

Iwapo atarejea Angola, pia anaweza kukamatwa – kwa amri ya serikali, Interpol imetoa hati ya ombi la kukamatwa kwake, hata hivyo si hati ya kimataifa ya kukamatwa.

Dos Santos amesema baada ya miaka hii migumu na mali zake kuzuiliwa, sasa anataka watu wasikie upande wa simulizi yake “tata” “kwa matumaini ya kuanza kufafanua dhana potofu zilizopo”.

Watu wawili wauawa na mwanafunzi wa kike kwa kupigwa risasi katika shule ya Kikristo Marekani

.

Mwanafunzi mmoja amefyatua risasi katika shule ya kibinafsi ya Kikristo katika jimbo la Wisconsin Marekani, na kujeruhi watu sita na kumuua mwalimu na mwanafunzi kijana.

Mkuu wa Polisi wa Madison Shon Barnes alimtaja mshambuliaji huyo Jumatatu usiku kuwa mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 15 katika shule hiyo.

Mamlaka inasema mshambuliaji huyo alikuwa shule ya Abundant Life Christian School kabla ya kufyatua risasi na alikutwa amefariki katika eneo la tukio.

Wanafunzi sita walijeruhiwa, wakiwemo wawili waliopata majeraha yanayo tishia maisha yao.

Mwanafunzi wa gredi ya pili alikuwa wa kwanza kupiga simu, kulingana na Mkuu wa Polisi Barnes.

“Leo ni siku ya huzuni sio tu kwa Madison, kwa nchi yetu yote,” Barnes alisema.

Aliongeza kuwa polisi hawajabaini sababu za tukio hilo la ufyatuaji risasi, na familia ya mshukiwa ilikuwa ikishirikiana na uchunguzi.

Alisema bado haijabainika jinsi mshambuliaji huyo alipata bunduki.

Hata hivyo, matukio ya ufyatuaji risasi kwa wingi na wanawake ni nadra na ufyatuaji risasi shuleni unaofanywa na washambuliaji wa kike ni vigumu sana kutokea.

Athari za kimbunga huko Mayotte ni kama matokeo ya vita vya nyuklia – wakaazi

.

Wakaazi wa eneo laMayotte wamezungumza juu ya “athari za kimbunga” kibaya zaidi katika miaka 90 ambacho kilipiga eneo la Bahari ya Hindi ya Ufaransa.

Kimbunga Chido kiliwasili kwa kasi ya upepo zaidi ya 225km/h (140mph), katika maeneo yenye tambarare ambapo wengi wanaoishi huko wanakumbwa na lindi la umaskini.

“Hatujapata maji kwa siku tatu sasa,” mkazi mmoja wa mji mkuu wa Mamoudzou alisema. “Baadhi ya majirani zangu wana njaa na kiu,” mwingine alisema.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema atasafiri hadi Mayotte “katika siku zijazo”, huku akiahidi kusaidia raia wake, wafanyikazi wa umma na huduma za dharura zinazohusika katika juhudi za uokoaji.

Iran yasitisha sheria mpya yenye utata ya kanuni za mavazi

.

Baraza la Usalama la Taifa la Iran limesitisha utekelezaji wa “sheria ya hijabu na kutokuwa na mahusiano yoyote ya ngono kabla ya ndoa,” ambayo ilikuwa ianze kutekelezwa siku ya Ijumaa.

Rais Massoud Pezeshkian aliita sheria hiyo “yenye utata na inayohitaji marekebisho”, akiashiria nia yake ya kutathmini upya hatua zake.

Sheria mpya iliyopendekezwa – ambayo ingeleta adhabu kali zaidi kwa wanawake na wasichana kwa kutofunika nywele zao, kuonyesha mapaja au sehemu ya chini ya miguu – ilikuwa imekosolewa vikali na wanaharakati wanaotetea haki za kibinadamu.

Kanuni kali za mavazi zilizowekwa kwa wanawake na wasichana, ambazo zimechukuliwa kama kipaumbele cha usalama wa taifa na watawala wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa miongo kadhaa, zilisababisha maandamano siku za nyuma.

Chini ya sheria hiyo mpya, wahalifu wanaorudia makosa na yeyote aliyekejeli sheria hizo atakabiliwa na faini kubwa zaidi na kifungo cha muda mrefu cha hadi miaka 15 jela.

Pia inaamuru kwamba biashara ziripoti mtu yeyote anayekiuka sheria.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalionyesha wasiwasi wake.

Amnesty International ilisema mamlaka za Irani “zinatafuta kuimarisha mfumo wa ukandamizaji ambao tayari unakera wengi”.

Wakati wa uchaguzi wa rais mwezi Julai, mgombea wa wakati huo Pezeshkian alikosoa waziwazi jinsi wanawake wa Iran wanavyotendewa kuhusu suala la kuvaa hijabu.

Aliahidi kutoingilia maisha yao ya kibinafsi, msimamo ambao uliwagusa Wairani wengi, haswa kutoka kwa kizazi kipya kilichokatishwa tamaa na udhibiti mkali wa serikali.

Mvutano unaozingira vazi la Hijabu umeendelea kuwa mkubwa tangu maandamano ya nchi nzima mwaka 2022 yaliyochochewa na kifo cha Mahsa “Zhina” Amini, msichana wa Kikurdi aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi baada ya kuzuiliwa kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, vijana wengi wa kike wa Kiirani wamevua hijabu zao kwa ukaidi hadharani, wakipinga mamlaka ya serikali.

Assad asema hakuwa na nia ya kuondoka Syria – taarifa inadai

.

Rais wa zamani wa Syria Bashar al-Assad anasema hakuwahi kukusudia kukimbilia Urusi – katika kile kinachodaiwa kuwa kauli yake ya kwanza tangu kuanguka kwa utawala wake siku nane zilizopita.

Taarifa ya Assad iliripotiwa kuwekwa kwenye mtandao wa Telegram katika akaunti inayomilikiwa na rais wa Syria siku ya Jumatatu, ingawa haijabainika ni nani anayeidhibiti kwa sasa – au ikiwa aliandika ujumbe huo mwenyewe.

Ndani yake inasema kwamba, mji mkuu wa Syria ulipoangukia mikononi mwa waasi, alikwenda katika kambi ya kijeshi ya Urusi katika jimbo la Latakia “kusimamia operesheni za mapigano” na hapo ndipo alipoona kwamba wanajeshi wa Syria wameacha nyadhifa zao.

Kambi ya kijeshi ya Hmeimim pia ilikuwa chini ya “mashambulizi makali ya ndege zisizo na rubani” na Warusi waliamua kumsafirisha kwa ndege hadi Moscow, anasema.

Katika taarifa hiyo – iliyochapishwa kwa Kiarabu na Kiingereza – kiongozi wa zamani wa Syria anaripotiwa kuelezea kile kilichotokea tarehe 8 Disemba.

“Bila kuwa na njia madhubuti ya kuondoka kwenye kituo hicho cha kijeshi, Moscow iliomba amri kambi hiyo ipange kumhamisha mara moja hadi Urusi jioni ya Jumapili tarehe 8 Desemba,” taarifa hiyo ilisema.

“Hii ilitokea siku moja baada ya kuporomoka kwa Damascus, kufuatia kuanguka kwa nafasi za mwisho za kijeshi na kusababisha taasisi zote kusitisha shughuli zake.”

Assad hakuonekana popote pale wakati miji au majimbo ya Syria yakiangukia mikononi mwa waasi wanaoongozwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu Hayat Tahrir al-Sham (HTS) ndani ya muda wa siku 12.

Hata hivyo, uvumi uliongezeka kuwa aliikimbia nchi kwani hata waziri mkuu wake hakuweza kuwasiliana naye wakati wa msako wa waasi kuelekea Damascus.

Mnamo tarehe 9 Disemba, vyombo vya habari vya Urusi vilitangaza kwamba amepewa hifadhi huko – ingawa hakujawa na uthibitisho wowote rasmi.

enerali wa Urusi auawa katika mlipuko mjini Moscow

.

Jenerali wa ngazi za juu katika jeshi la Urusi ameuawa katika mlipuko uliotokea mjini Moscow.

Luteni Jenerali Igor Kirillov, mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Nyuklia, Biolojia, Kemikali (NBC), alikuwa akiondoka kwenye makazi yake mapema Jumanne wakati kifaa kilichofichwa kwenye skuta kilipolipulika, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi ilisema.

Iliongeza kuwa msaidizi wa Kirillov pia aliuawa.

Mnamo mwezi Oktoba, Uingereza iliweka vikwazo kwa Kirillov, ikisema alikuwa amesimamia matumizi ya silaha za kemikali nchini Ukraine na alikuwa kiungo muhimu kama “msemaji wa habari za Kremlin”.

Siku ya Jumatatu, idara ya siri ya Ukraine, SBU, ilimfungulia mashtaka bila kuwepo mahakamani, ikisema kwenye Telegram “alihusika na matumizi makubwa ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku”.

Kamati ya Uchunguzi, mamlaka kuu ya uchunguzi ya Urusi, ilisema “imefungua kesi ya jinai ya mauaji ya wanajeshi wawili”.

“Wataalam wa uchunguzi na huduma za uendeshaji wapo katika eneo la tukio,” ilisema.

“Hatua za uchunguzi na shughuli za upekuzi zinafanywa kwa lengo la kubaini hali zote za uhalifu.”

Ukraine yakiri kumuua Jenerali wa kikosi cha nyuklia wa Urusi

df
Maelezo ya picha,Luteni Jenerali Igor Kirillov

Vyanzo vya BBC katika idara za usalama za Ukraine vinadai kuwa Ukraine ndio imehusika na operesheni ya kumuua Igor Kirillov mjini Moscow.

Kulingana na chanzo hicho, pikipiki iliyokuwa na vilipuzi ililipuliwa wakati Kirillov na msaidizi wake wakikaribia jengo moja huko Moscow asubuhi ya leo.

Chanzo hicho kinadai Kirillov ni “mlengwa halali” kwa vile alikuwa mhalifu wa kivita ambaye alitoa amri ya kutumia silaha za kemikali zilizopigwa marufuku dhidi ya jeshi la Ukraine.

Luteni Jenerali Kirillov alikuwa akisimamia vikosi vya ulinzi vya nyuklia vya Urusi – Vikosi vya Ulinzi vya Nyuklia, Baiolojia na Kemikali.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment