Joe Biden atoa msamaha kwa watu 39 na kupunguza adhabu kwa watu 1,500

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Joe Biden ametangaza siku ya Alhamisi Desemba 12, 2024 kwamba ametoa msamaha kwa watu 39 na kupunguza adhabu kwa karibu watu 1,500.

Rais wa MarekaniJoe Biden wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mnamo Desemba 8, 2024.
Rais wa MarekaniJoe Biden wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mnamo Desemba 8, 2024. REUTERS – Ken Cedeno

“Ninawasamehe watu 39 ambao wamejirekebisha na kujutia makosa yao,” Bw. Biden amesema katika taarifa yake, akiongeza kuwa pia amepunguza adhabu “kwa karibu watu 1,500 wanaotumikia vifungo virefu gerezani.” “Marekani imejengwa juu ya ahadi ya uwezekano na nafasi ya pili,” Joe Biden ameongeza. “Kama rais, nina mamlaka ya kuwasamehe watu ambao wamejutia makosa yao na wakajirekebisha.”

Marais wa Marekani huamuru mamia ya msamaha au kupunguza adhabu, na kuongeza kasi kubwa mwishoni mwa mamlaka yao ya miaka minne. Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, hii ndiyo idadi kubwa zaidi ya vitendo vya huruma katika siku moja katika historia yote ya Marekani na watu 1,500 wanaohusika walikuwa wakitumikia vifungo vyao nyumbani kwa angalau mwaka mmoja.

Watu hawa waliowekwa kizuizini nyumbani “wakati wa janga la Covid wameweza kuungana tena katika familia zao na jamii na wameonyesha kuwa wanastahili nafasi ya pili,” ameongeza rais anaye maliza muda wake. Joe Biden pia amebainisha kuwa watu 39 waliosamehewa kwa hukumu zinazohusiana na vitendo visivyo vya ukatili “walijitolea kuifanya jumuiya yao kuwa imara na salama”.

Miongoni mwa walioathiriwa na uamuzi huo Alhamisi ni “mpiganaji wa zamani na rubani ambaye anatumia wakati wake mwingi kusaidia waumini wa kanisa lake,” Ikulu ya White House imesema. Muuguzi “ambaye ameongoza majibu ya dharura wakati wa majanga kadhaa ya asili” na mshauri wa madawa ya kulevya “ambaye anafanya kazi kwa hiari” pia wako kwenye orodha ya watu hao waliopewa msmaha wa rais, chanzo hicho kimeongeza.

Mwanzoni mwa Desemba, Joe Biden hatimaye alirejea ahadi yake kwa kumsamehe mtoto wake Hunter, ambaye alikuwa akisubiri hukumu yake katika kesi za kumiliki silaha kinyume cha sheria na kukwepa kulipa kodi. Kiongozi huyo wa Marekani hata hivyo alikuwa amehakikisha mara kadhaa kwamba hatatoa msamaha wa rais kwa mwanawe. Hivi majuzi mnamo Septemba, Ikulu ya White House ilithibitisha hili.

Mtangulizi wake na mrithi wa hivi karibuni kutoka cama cha Republican Donald Trump pia alisamehe mnamo Desemba 2020 baba ya mkwe wake na mshauri Jared Kushner, Charles Kushner, alihukumiwa mwaka wa 2004 kifungo cha miaka miwili jela kwa ufujaji wa kodi. Hivi majuzi alitangaza nia yake ya kumteua katika wadhifa wa kifahari wa balozi mjini Paris.

Bill Clinton, mwaka wa 2001, katika siku ya mwisho ya mamlaka yake, alimsamehe kaka yake wa kambo Roger Clinton, aliyepatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya cocaine mwaka wa 1985. Katika kesi ya Roger Clinton na Charles Kushner, wanaume wote wawili walikuwa wametumikia vifungo vyao gerezani wakati wa msamaha wa rais.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment