Afrika Leo Mchana-Cantona Joseph

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja

Muhtasari

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Mchana ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 13/12/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Aliyekuwa mkuu wa gereza la Syria ashtakiwa Marekani kwa kutesa watu

.

Afisa wa zamani wa serikali ya Syria ameshtakiwa nchini Marekani kwa kutesa watu, mamlaka ilisema Alhamisi.

Samir Ousman Alsheikh, ambaye alisimamia Gereza Kuu la Damascus kuanzia 2005 na 2008, alishtakiwa kwa makosa kadhaa ya kusababisha mateso na njama ya kutesa wafungwa.

Mamlaka ya Marekani ilisema madai dhidi ya Alsheikh yalikuwa “ya kuogofya”.

Alikamatwa mapema mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles (LAX) kwa mashtaka mawili ya ulaghai wa uhamiaji, na alikuwa amenunua tikiti ya kwenda pekee kutoka LAX hadi Beirut, Lebanon.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani, Wilaya ya Kati ya California, Alsheikh alificha kazi yake katika gereza hilo na akakanusha kutesa mtu yeyote katika maombi yake ya viza ya Marekani na uraia.

Maafisa wa Marekani wanasema Alsheikh yeye binafsi alisababisha “maumivu makali ya kimwili na kiakili na mateso kwa wafungwa wa kisiasa na wengine” katika nafasi yake chini ya rais aliyepinduliwa Bashar al-Assad.

Inadaiwa aliamuru wafungwa “Kupelekwa eneo la Adhabu” katika gereza hilo, ambapo wangepigwa wakiwa wamesimamishwa juu ya dari na kuwekewa kifaa ambacho kingeweza kusababisha “maumivu makali”, wakati mwingine kusababisha kuvunjika kwa mgongo.

“Takriban miaka 20 iliyopita, mshtakiwa alishtakiwa kwa kuwatesa wafungwa nchini Syria na, leo, tuko hatua moja karibu zaidi ya kumwajibisha kwa uhalifu huo mbaya”, Afisa Maalum Msimamizi wa ofisi ya HSI Los Angeles, Eddy Wang, alisema katika taarifa.

Shirika la Reli Tanzania kununua injini za dizeli kupiga jeki shughuli za SGR

g
Maelezo ya picha,Kituo cha treni ya umeme Dar es Salaam kimeundwa kufanana na madini ya tanzanaiti

Shirika la reli nchini Tanzania (TRC) limesema litanunua injini zinazotumia dizeli ili kupiga jeki shughuli za usafiri wa leri nchini humo.

Hatua hii inalenga kukabiliana na tatizo la kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme kunakoyakumba maeneo mengi ya nchi hiyo.

”Fedha za injini tayari zimetengwa katika bajeti yetu. Mchakao wa ununuzi unaendelea na tunatarajia kupata injini mwaka ujao”, amesema Masanja kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini Tanzania.

Hivi karibuni ulifanyika uzinduzi reli ya umeme na jengo kama madini adimu ya tanzanite, jijini Dar es Salaam, kuashiria mwanzo mpya katika sekta hiyo ya safari reli nchini Tanzania.

Treni zinazotumia umeme nchini Tanzania, hubeba abiria kutoka mji wa kibiashara Dar es Salaam hadi mji mkuu, Dodoma, kwa safari ya chini ya saa nne, nusu ya muda ukisafi kwa barabara.

Ujenzi huo wa Reli ya Standard Gauge (SGR) yenye urefu wa kilomita 2,560 (maili 1,590) inayotarajiwa kuunganisha miji muhimu na kuunganisha nchi jirani Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Raila kukabiliana na washindani wawili wa kiti cha AU katika mdahalo leo TV

g

Wagombea wa Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika wanatarajiwa kukabiliana leo ana kwa ana katika mdahalo kuonyesha uwezo wao wa kazi hiyo itakapotimia saa moja kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki .

Mdahalo huo kuhusu Afrika utafanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa.

Miongoni mwa wanaoshiriki ni mgombea wa Kenya katika nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), Raila Odinga.

Kwenye mdahalo huo Raila atakuwa pamoja na wagombeaji wengine wawili; Waziri wa mambo ya jje wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascr Richard Randriamandrato. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius Anil Kumarsingh Gayan, alijiondoa mapema mwezi huo.

AU inasema Mdahalo wa Afrika ni jukwaa la wagombea kuhutubia raia wa Afrika katika mdahalo wa televisheni, unaorushwa moja kwa moja. Wagombea watawasilisha maono na mawazo yao juu ya utekelezaji wa Ajenda 2063 ya AU.

“Mjadala unaangazia masuala ya sera na ushiriki wenye mwelekeo wa suluhu kuhusu jinsi kila mgombea anavyopanga kuendeleza utimilifu wa matarajio na malengo ya jjenda ya 2063, miradi mingine ya AU yenye mwelekeo wa bara, na misimamo ya pamoja ya Afrika,” AUC inasema.

Trump ‘apinga vikali’ Ukraine kurusha makombora ndani kabisa ya Urusi

g

Rais mteule Donald Trump amesema ‘hakubaliani kabisa’ na suala la Ukraine kurusha makombora yaliyotolewa na Marekani ndani ya Urusi.

Katika mahojiano siku ya Alhamisi Trump alisisitiza kuwa Marekani hataiacha Ukraine kwani uungaji mkono wa Marekani kwa Kyiv ni njia kuu katika juhudi za kumaliza vita.

Washington imepeleka makombora yake ya masafa marefu ya ATACMS kwa Ukraine ambayo yanaweza kupenya ndani ya Urusi, na kusababisha ulipizaji kisasi kutoka kwa Moscow ambayo imejibu kwa kombora lake jipya la hypersonic.

“Napinga vikali kutuma makombora mamia ya maili nchini Urusi. Kwa nini tunafanya hivyo?” alisema katika mahojiano na jarida la Time ambalo lilimtaja kuwa “mtu bora wa mwaka” mnamo Alhamisi.

Makombora ya ATACMS yana uwezo wa juu wa kushambulia maili 190 (kilomita 300) kulingana na data inayopatikana kwa umma.

azama: Mshukiwa wa uhalifu alivyokwama kwenye bomba la moshi wakati alipokuwa akiwatoroka polisi

Maelezo ya video,Tazama: Mwanamume anayejaribu kuwatoroka polisi anakwama kwenye bomba la moshi

Mwanamume mmoja huko Fall River, Massachusetts, ambaye alikimbia kupitia paa kutoka kwa polisi wa kutekeleza agizo la upekuzi, ameokolewa baada ya kukwama kwenye bomba la moshi.

Picha za kamera kutoka kwa Idara ya Polisi ya Jiji la Fall River zinaonyesha wapelelezi wakimgundua Robert Langlais mwenye umri wa miaka 33 na kuomba usaidizi kutoka kwa idara ya zimamoto ili kumwachilia.

Langlais alipelekwa hospitali na baadaye alikamatwa kwa tuhuma za dawa za kulevya.

Hatma ya Rais wa Korea Kusini yakaribia huku wabunge wakipata vitisho vya kuuawa

g
Maelezo ya picha,Rais Yoon Suk Yeol aliushangaza ulimwengu kwa jaribio lake la kuweka sheria ya kijeshi

Rais Yoon Suk Yeol alishangaza ulimwengu kwa jaribio lake la kuweka sheria ya kijeshi

Habari zinakwenda haraka sana nchini Korea Kusini, na sasa magazeti hayawezi kuendelea kuchapishwakama kawaida . Jaribio la kushtukiza la Rais Yoon Suk Yeol la kulazimisha sheria ya kijeshi usiku wa Jumanne iliyopita lilikuwa la muda mfupi kiasi kwamba lilishindwa kuchapishwa kwenye ukurasa wa mbele.

Kufikia wakati alipowawasambaza askari, vyombo vya habari vilikuwa tayari vimechapisha. Kufikia muda wa matoleo ya magazeti ya siku iliyofuata, unyakuzi mamlaka wa nguvu ulioshindwa ulikuwa tayari umeshindwa.

Ndani ya wiki moja, rais amebadilika kutoka kuwa na majuto na kuomba msamaha, akitumai kukwepa kushtakiwa, hadi kuwa mkaidi wa hali ya juu, akiapa kupigana hadi mwisho huku hatma yake ikikaribia.

Amepigwa marufuku kuondoka nchini huku akichunguzwa kwa uhaini ambao ni uhalifu unaostahili adhabu ya kifo na anakabiliwa na kura ya pili ya kuondolewa mashitaka mwishoni mwa juma hili, huku uungwaji mkono kutoka kwa chama chake ukizidi kupungua. Wakati huohuo, kuna hasira kubwa kutoka kwa maelfu ya watu mitaani kila siku inazidi kuongezeka.

Kwa muda mfupi wiki hii ilionekana kana kwamba alikuwa ameafikiana na chama chake kujiuzulu mapema, ili wasimtoe madarakani katika kura ya Jumamosi iliyopita. Lakini wiki ilipozidi kwenda, hakukuwa na dalili ya rais wala maelezo ya mpango huo.

Hili limewaacha kila mtu na swali lile lile, swali kubwa – ni nani anayeendesha nchi?

g
Maelezo ya picha,Rais Yoon Suk Yeol

Ili kupitishwa kwa hatua ya kumuondolewa mashtaka, ni lazima theluthi mbili ya wabunge wapige kura ya ndio, ikimaanisha kuwa wabunge wanane wa chama tawala lazima wajiunge na upinzani. Ni wachache hadi sasa wametangaza nia yao ya kufanya hivyo.

Mmoja wa watu waliokua wa kwanza kubadilisha mawazo yake alikuwa Kim Sang-wook. “Rais hana sifa tena za kuongoza nchi, hafai kabisa,” aliiambia BBC kutoka ofisi yake ya bunge la taifa.

Katika eneo bunge lake la kihafidhina, Kim alisema alipokea vitisho vya kuuawa kwa kubadili upande wake. “Chama changu na wafuasi wameniita msaliti,” alisema, akitaja siasa za Korea Kusini kama “za kikabila sana”.

Kiongozi wa Uganda aunga mkono kesi za kijeshi huku mpinzani wake akiwekwa gerezani wakati wa Krismasi

g
Maelezo ya picha,Rais Yoweri Museveni, ambaye alisifu mahakama za kijeshi kwa kuchangia amani ya taifa hilo la Afrika Mashariki, amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 80 ametetea matumizi ya mahakama za kijeshi kuwashitaki raia, kufuatia malalamiko ya kukamatwa na kushtakiwa kwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Besigye mwenye umri wa miaka 68 ameshtakiwa katika mahakama ya kijeshi kwa kumiliki bastola na kujaribu kununua silaha nje ya nchi, madai ambayo anayakanusha.

Besigye, ambaye alitekwa nyara wakati alipozuru Kenya mwezi uliopita na kupelekwa Uganda kwa nguvu, aligundua Jumanne kwamba atasherehekea Krismasi akiwa kizuizini kwa kuwa kesi yake imeahirishwa hadi mwezi Januari.

Museveni alisema uhalifu wowote unaohusisha bunduki unashughulikiwa katika mahakama ya kijeshi ili kuhakikisha utulivu wa nchi hiyo kwa kuwa mahakama za kiraia zinachukua muda mrefu kushughulikia kesi.

Mamia ya raia wameshtakiwa katika mahakama za kijeshi nchini Uganda, licha ya kwamba mahakama ya katiba imetoa uamuzi dhidi ya kuendeshwa kwa kesi za raia katika mahakama za kijeshi.

“Nimeona hoja katika makaratasi ya baadhi ya wanasheria kuhusu usahihi wa baadhi ya raia kufikishwa katika mahakama ya kijeshi,” Rais Museveni alisema katika ujumbe mrefu wa X.

Alisema chama chake cha National Resistance Movement (NRM) kilitunga sheria kupitia bunge mwaka 2005 kuruhusu matumizi ya mahakama za kijeshi kwasababu ya “shughuli za uhalifu na magaidi ambazo zilihusisha matumizi ya bunduki kuua watu kiholela’’.

Besigye amepinga kushtakiwa na mahakama akisema kuwa kama kuna mashtaka yoyote dhidi yake, anapaswa kushtakiwa katika mahakama ya kiraia.

Lazima Nato ibadili mawazo kuwa ya wakati wa vita, aonya katibu mkuu

g
Maelezo ya picha,Mark Rutte aliitaja hali ya sasa ya usalama kuwa “mbaya zaidi katika maisha yangu”

Mkuu wa Nato amesema ni wakati wa “kujitosa katika fikra za wakati wa vita”, huku akiwaonya wanachama wa muungano huo wa kijeshi kuwa hawatumii matumizi yao vya kutosha kujiandaa kwa tisho la mzozo wa baadaye na Urusi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Mark Rutte amesema Moscow “inajiandaa kwa mapambano ya muda mrefu na Ukraine na sisi”, akielezea hali ya sasa ya usalama kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika maisha yake.

“Hatuko tayari kwa kile kinachokuja katika kipindi cha miaka minne hadi mitano,” alisema katika hotuba yake ya kwanza kubwa tangu awe katibu mkuu mwezi Oktoba, akiwataka wanachama “kupunguza” matumizi yao ya ulinzi.

Matamshi yake yanakuja wiki kadhaa kabla ya rais mteule Donald Trump kuingia madarakani, baada ya kusema awali kuwa Marekani haitawalinda washirika wa Nato ambao wameshindwa kutumia fedha za kutosha katika ulinzi.

Wanachama wa Nato wameahidi kutumia angalau 2% ya thamani ya uchumi wao na pato la taifa kwa ajili ya ulinzi kwa mwaka na 2024.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment