Zaidi ya watu 100 wauawa katika shambulio la jeshi katika soko nchini Sudani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Zaidi ya watu 100 waliuawa Jumatatu katika shambulio la jeshi kwenye soko lililojaa watu huko Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudani katika eneo linalodhibitiwa na wanamgambo, kundi la wanasheria nchini Sudani limesema siku ya Jumanne Desemba 10, 2024.

Picha hii iliyopigwa tarehe 1 Septemba 2023 inaonyesha uharibifu katika eneo la soko la ng'ombe huko el-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini mwa Sudan.
Picha hii iliyopigwa tarehe 1 Septemba 2023 inaonyesha uharibifu katika eneo la soko la ng’ombe huko el-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini mwa Sudan. AFP – –

Shambulio hilo baya, ambalo jeshi linakanusha khusika, lilifanyika Kabkabiya, takriban kilomita 180 magharibi mwa El-Facher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, uliozingirwa tangu mwezi Mei na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (FSR), kundi hilo la wanasheria, Emergency Lawyers, limesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Kundi hili la wanasheria wanaounga mkono demokrasia linaandika ukatili uliofanywa tangu kuanza kwa vita kati ya jeshi la kawaida na RSF, miezi 20 iliyopita. Mzozo ambao umesababisha makumi ya maelfu ya watu kupoteza maisha na zaidi ya milioni kumi na moja kukimbia makazi yao, na kuchochea moja ya machafuko mabaya zaidi ya hivi karibuni ya kibinadamu, kulingana na Umoja wa Mataifa.

“Shambulio hilo lilitokea katika siku ya soko ya kila juma ya jiji hilo, ambapo wakazi kutoka vijiji mbalimbali jirani walikuwa wamekusanyika kufanya biashara zao,” na kusababisha vifo vya “zaidi ya watu 100” na kujeruhi “mamia ya watu wengine, wakiwemo wanawake na watoto,” kulingana na shirika hilo. “Shambulio (la jeshi) lilifanywa kwa makusudi katika maeneo ya makazi yenye watu wengi,” wanashutumu.

Jeshi la Sudani kwa upande wake limekanusha kufanya shambulio hili, likilaani katika taarifa kwa vyombo vya habari “uongo” unaoenezwa na vyama vya siasa vinavyounga mkono RSF, na kuongeza kuwa litaendelea “kutumia haki yake halali ya kulinda nchi”.

Darfur, eneo lenye ukubwa wa Ufaransa, ni makazi ya takriban robo ya wakazi wa Sudani, lakini zaidi ya nusu ya watu wake milioni 10 wameyahama makazi yao. Mwezi Julai, ripoti inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilisema njaa ilienea katika kambi kubwa ya wakimbizi huko Darfur Kaskazini baada ya kuzingirwa kwa miezi kadhaa na RSF ambayo ilizuia takriban biashara zote na upatikanaji wa msaada.

Hivi majuzi kundi la wanasheria, Emergency Lawyers, waliripoti matukio kadhaa nchini humo, ikiwa ni pamoja na kuanguka kwa ndege isiyo na rubani isiyojulikana mnamo Novemba 26 huko Kordofan Kaskazini, Sudan ya kati, na kusababisha vifo vya watu sita. Jeshi la serikali, likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, na RSF ya mshirika wake wa zamani na makamu, Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, wameshutumiwa kwa kuwalenga raia kimakusudi na kulipua ovyo maeneo ya makazi tangu kuanza kwa mzozo kati yao, mnamo mezi Aprili 2023.

Siku ya Jumanne, shirika la Human Rights Watch ilimeshutumu RSF na washirika wake, wanamgambo wa Kiarabu kwa kufanya dhuluma nyingi dhidi ya raia katika jimbo la Kordofan Kusini kati ya mwezi wa Desemba 2023 na Machi 2024. HRW ilishutumu “uhalifu wa vita” wa makundi haya, ikiwa ni pamoja na “mauaji,” ubakaji na utekaji nyara wa wakaazi wa kabila la Nuba, pamoja na “uporaji na uharibifu wa nyumba”, na kuutaka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kupeleka ujumbe wa kulinda raia nchini Sudani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment