Amnesty inalishutumu jeshi la DRC kwa ‘uhalifu dhidi ya ubinadamu’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International linasema limekusanya ushahidi wa “uhalifu unaowezekana dhidi ya ubinadamu” uliofanywa na jeshi la Kongo wakati wa mauaji ya takriban watu 56 mnamo mwaka 2023.

Watu waliokamatwa kabla ya maandamano ya kikundi cha kidini dhidi ya MONUSCO, Agosti 30, 2023.
Watu waliokamatwa kabla ya maandamano ya kikundi cha kidini dhidi ya MONUSCO, Agosti 30, 2023. © AFP

Amnesty International katika ripoti iliyochapishwa siku ya Jumatano imeshutumu maafisa wakuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) kwa “uhalifu unaowezekana dhidi ya ubinadamu” wakati wa mauaji ya watu 56 huko Goma mnamo mwaka 2023.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali, “vikosi vya usalama vya Kongo vilijihusisha na mauaji” kwa kuwafyatulia risasi waandamanaji mnamo Agosti 30, 2023 huko Goma, mji mkuu wamkoa wa Kivu Kaskazini (mashariki), eneo linalokabiliwa na ghasia za makundi yenye silaha kwa zaidi ya miaka thelathini.

Maandamano dhidi ya MINUSCO

“Takriban watu 56 waliuawa kinyume cha sheria na zaidi ya 80 kujeruhiwa,” Amnesty inasema. Wengi wa wahanga walikuwa wa vuguvugu la kidini-fumbo, Imani ya Kiyahudi na Masihi kuelekea Mataifa (FNJMN), ambayo kiongozi wake aliitisha maandamano dhidi ya MiINUSCO (Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini DRC).

Shirika hilo linasema “limewatambua maafisa watatu wa jeshi ambao wanapaswa kuchunguzwa kibinafsi na, ikiwa ushahidi wa kutosha utapatikana, kufunguliwa mashtaka kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.”

Kwa mujibu wa Amnesty, hawa ni Constant Ndima Kongba, aliyekuwa gavana wa kijeshi wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Kanali Mike Mikombe Kalamba, Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Jamhuri, na Meja Peter Kabwe Ngandu, aliyekuwa naibu wake wakati wa operesheni hiyo mbaya.

Hukumu ya kifo

Mnamo mwezi wa Oktoba 2023, mahakama ya Kongo ilimhukumu Kanali Mike Mikombe na wanajeshi wengine watatu kifungo cha miaka kumi jela kwa “mauaji”. Amnesty International pia inatoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufungua “bila kuchelewesha uchunguzi huru kuhusu jukumu la MINUSCO, hasa usimamizi wake, na kufanya hitimisho kwa umma”.

“Ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa iliyoshauriwa na Amnesty International ilithibitisha idadi ya vifo kuwa 102” ikiwa ni pamoja na “wanaume 90, wanawake wanane na wavulana wanne, na zaidi ya 80 waliojeruhiwa,” kulingana na waandishi wa ripoti hiyo. FNJMN iliihakikishia shirika la habari la AFP mnamo Agosti 30, 2024 kwamba ilikuwa imethibitisha hesabu ya watu 103 waliouawa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment