Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kipimo mojawapo ya Mafanikio yetu 2023 ni jinsi tunavyotumia muda wetu, “TIME MANAGEMENT”. Kama unachangamoto ya Ku-manage muda basi tumia hizi mbinu kutoka kwa, “BRIAN TRACY”.
1. GOALS.
• Bila kuwa na malengo utatumia muda wako vibaya.Brian asema, “Jiulize Wewe Nani, unataka nini, na wapi unataka kufika na malengo yako ni yapi katika Maisha, familia, kazi biashara na Binafsi?”
2. ORGANIZED PLAN OF ACTION.
• Watu wengi wana malengo ila hawajaweka mipango ya kutekeleza. Brian anasema, “Weka mipango na mikakati dhabiti ya kufikia malengo yako”.
3. MAKE A LIST
• Brian anasema, “Kila siku jioni andaa orodha ya siku yako inayofuata. Itakusaidia kutumia muda wako vizuri”
4. SET PRIORITIES
• Kila ainisha vitu unavyotakiwa kufanya kulingana na Umuhimu na thamani yake. Anza na vitu vya msingi zaidi alafu vya ziada baadaye.
5. CONCETRATION
• Jijengee Nidhamu ya ku-FOCUS katika jambo moja Hadi kulimaliza. Usiguse huku na kule mwishowe hakuna ulichotimiza.
6. DEADLINES
• Katika kila kitu unachokifanya jiwekee ukomo wa muda unaotakiwa kutumia ili uweze kujipima vizuri. Kwenye kazi au biashara jitahidi kufikia deadlines zako mapema.
7. TIME LOG (TRACKING).
• Jenga Nidhamu ya kurekodi jinsi unavyotumia muda wako. Nini huwa kinakula muda wako Sana, na je inastahili?
• Huwa unapimaje muda wako?
• Brian Tracy anasema kuwa, “Watu waliofanikiwa hupima muda wao kwa dakika. Watu wa kawaida hupima muda wao kwa masaa, siku na wiki. Alafu watu wa chini kabisa hupima muda wao kwa asubuhi, Mchana na jioni”.
8. PROCRASTINATION
• Jitahidi sana kuepuka kughairisha vitu vya msingi Kwa sababu ya kufanya vitu visivyo na muhimu.
9. DELEGATE
• Wape watu wengine yale majuku yako Madogo madogo ili uweze Ku-Focus na vitu muhimu na vyenye tija na THAMANI kubwa.
10. MEETINGS
• Epuka vikao visivyo vya lazima. Usihudhurie kikao bila kujua Ajenda
zake. Kama unaweza kumtuma mwakilishi, mtume.
11. KEY RESULTS AREA.
• Jua nini kinatarajiwa kutoka kwako ili kuipa muda wako thamani ya kufanya hicho kitu.
12. BATCHING TASKS
• Fanya baadhi ya vitu kwa pamoja badala ya kuchanganya changaya. Mf. Piga simu zote Kwa wakati mmoja.
13. NEATNESS
• Tafiti zinasema, eneo la Kazi lenye mpangilio mzuri huchochea ufanisi na Productivity. panga vitu vizuri.
14. EXTRA GROWTH TIME
• Kuwa na muda wa ziada wa kujinoa ili kuwa Bora zaidi. Brian anasema, “Unalipwa kulingana na thamani unayotoa siyo muda unayotumia”.
15. PANCTUALITY.
• BE ON TIME. Tokea kwa wakati, usichomeshe watu mahindi. Heshimu miadi yako. Deliver kwa wakati.
16. SIMPLIFICATION
• Kila siku jitahidi kutafuta mbinu za kurahisha ufanyaji wa
mambo. Usitumie Nguvu na muda mwingi wakati kuna nyenzo rahisi zaidi.
17. TEAM WORK
• Kama kuna kazi ambayo inafanyika kwa Urahisi zaidi mkiwa kama timu, basi shirikisha watu. Usikomae Kwa masaa 20 mwenye wakati inaweza kufanywa Kwa masaa 5 na watu 4.
18. INTERRUPTIONS
• Chochote chenye kuingilia ratiba yako au muda wako jitahidi ku-control. Kama ni simu, Turn off data au notifications, tafuta utulivu na mwingiliano usio lazima.
19. NO
• Jifunze kusema hapana Kwa baadhi ya vitu na watu ili uweze kufanya vitu vya muhimu zaidi.
20. BALANCE
• Yote kwa yote kumbuka kuwa na Balance ya muda wako kwa kazi, biashara, familia, masomo, Afya na chochote kile unachokifanya katika Maisha yako.
Mwisho kabisa, Brian Tracy anasema kuwa, “Time Management is Life Management”.
Hivyo ukijua kutawala muda wako vizuri, basi umejua kuyawatala maisha yako vizuri.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.