Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Urusi, mshirika mkuu wa mamlaka ya Syria iliyong’olewa madarakani, ina kambi mbili za kijeshi nchini Syria na inajitahidi kuwahamisha waaasi na kuokoa kile kinachoweza kuokolewa. Chanzo kimoja huko Kremlin, kilichonukuliwa na mashirika ya Urusi, kinahakikisha kwamba waasi wamekubali kudhamini usalama wa kambi hizi, muhimu kwa operesheni barani Afrika.
Nchini Syria, waasi, wakiongozwa na kundi la Waislam wenye itikadi kali Hayat Tahrir al-Sham, waliuangusha utawala wa Rais Bashar al-Assad mnamo Desemba 7. Matukio haya yalikomesha miongo mitano ya utawala usiopingwa wa familia ya Assad. Rais huyo wa zamani ameikimbia nchi, mshirika mkuu wa Urusi ambayi iliingilia kijeshi nchini Syria tangu mwaka 2015, kumuunga mkono Bashar Al Assad. Kwa sasa Moscow ina kambi za kijeshi katika ardhi ya Syria.
Kulingana na habari iliyotumwa na vyombo vya habari vya Urusi, waasi “wamehakikisha usalama” wa kambi hizi. Msemaji wa Kremlin pia ameona ni “muhimu” kujadili na mamlaka ya baadaye ya Syria juu ya uwezekano wa matengenezo ya kambi ya jeshi la wanamaji la Urusi huko Tartous na uwanja wa ndege wa jeshi la Urusi huko Hmeimim.
Kambi “muhimu sana kwa operesheni Afrika”
“Hili ni suala la majadiliano na wale ambao watakuwa madarakani nchini Syria,” amesema, akibainisha kwamba Urusi inafanya “kila kitu kinachowezekana na kila kitu muhimu ili kuanzisha mawasiliano na wale ambao wanaweza kuwajibika kwa kuhakikisha usalama” wa kambi za kijeshi za Urusi nchini Syria.
Kambi hizi ni muhimu sana kwa shughuli za Urusi barani Afrika, haswa kituo cha anga cha Hmeimim, karibu na Latakia.
“Urusi inatumia kambi kadhaa nchini Syria, lakini kuna vituo vichache ambavyo ni muhimu zaidi, sio tu kwa operesheni nchini Syria, lakini pia kwa operesheni mahali pengine, pamoja na kambi za Latakia, Kambi ya wanahewa ya Hmeimim kwa mfano, na pia kambi ya jeshi la wanamaji ambayo inapatikana huko Tartous,” anabainisha Andrew Lebovich, mtafiti mshiriki katika Taasisi ya Clingendael.
“Kazi hizi ni muhimu sana, sio tu kwa operesheni nchini Syria, lakini pia kwa operesheni, kwa uhamisho wa wanajeshi na vifaa, kwa mfano nchini Libya, Sudani, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mali. Kwa hiyo kama, kwa mfano, hakutakuwa na kambi hizii nchini Syria, itafanya utaratibu wa uendeshaji wa shughuli barani Afrika kuwa mgumu zaidi, mgumu zaidi na pia wa gharama kubwa zaidi,” anaongeza mtafiti huyo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.