Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unataka Kuwa MWANAMKE Mwenye MAFANIKIO?…
i. Kukata Tamaa Kwasababu Ya Mambo Yaliyopita.
ii. Dependency Syndrome
iii. Kukosa Kujiamini (Lack of Self-belief)
iv. Emotional Instability (Kukosa Uimara wa Kihisia)
v. Kutokusamehe
vi. Kuambatana na Watu Wasio Sahihi (Wrong Association)
vii. Kutokuwa na Mpango wa Mafanikio ya Kifedha
Katika Makala Hii Tutazungumzia Njia Ya Saba
– Kutokuwa na Mpango wa Mafanikio ya Kifedha
Watu wengi sana hawana mpango wowote wa jinsi watakavyofanikiwa katika maisha hasa kifedha, mtaalamu wa masuala ya mafanikio…
…Brian Tracy anasema kuwa takribani 3% ya watu duniani hawana mpango wowote wa jinsi watakavyotimiza malengo yao. Kwa wanawake hili ni tatizo kubwa hata zaidi.
Labda nikuulize: Je, wewe una mpango wowote uliouweka wa kukusaidia kufanikiwa katika maisha yako?
Wanawake wengi sana wameshindwa kupiga hatua katika maisha yao kwa sababu wameamini kuwa maisha yao kuna siku yatabadilika yenyewe tu na hawahitaji kufanya chochote kile, hilo si kweli.
Kila mtu ambaye unamwona leo amepiga hatua katika maisha yake kuna siku alikaa chini na akapanga namna ya kupata matokeo ambayo leo anayo.
Bila kujali leo unafanya kazi ya namna gani, ama hauna kipato kabisa ni lazima ujiwekee mkakati wa nguvu wa namna unavyoweza kujikwamua kiuchumi katika maisha yako.
Katika mkakati wako unaweza kuweka malengo ya namna ambayo utatumia kipato chako kinachohusisha nguvu na muda wako (Active Income)
Ili uweze kuzalisha kipato ambacho kitaendelea kuingia hata wewe ukiwa haufanyi kazi yoyote ile (Passive Income).
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.