Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, wakati huu mjadala ukiendelea kuhusu katiba, viongozi wa upinzani Moise Katumbi na Martin Fayulu, wameweka misingi ya kutetea Katiba katika mkutano uliofanyika nchini Ubelgiji

Kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa Disemba mwaka uliopita, viongozi hawa wamekutana hapo jana ishara ya kuwa na lengo moja dhidi ya mapendekezo ya kugeuza katiba yanayotolewa na rais Felix Tshisekedi.
Mkutano huu wa Genval Ubelgiji unaleta kumbukumbu za 2016 ambapo walikutana tena kuunda harakati za kumuondoa madarakani rais wa wakati huo Joseph Kabila.

Wakati huu kambi ya Katumbi ikifurahishwa na hatua hii ya wawili hao kuja pamoja, msemaji wa chama cha Ensemble pour la République, Hervé Diakiese, amesema lengo la viongozi hawa wawili ni kutetea kanuni za katiba
Fayulu amesema hivi karibuni wataweka wazi hatua zao za pamoja, lakini kadhalika kabla ya mkutano huu alikutana na aliyekuwa muwaniaji wa urais Delly Sesanga nchini Ufaransa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.