Umoja wa mataifa waonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Sudan.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwa mara nyingine umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa na itakayoendelea kushuhudiwa nchini Sudan, wakati huu tayari hali ya njaa ikiwa imetangazwa kwenye taifa hilo.

Raia wakipanga foleni ili kujiandikisha kwa ajili ya utoaji wa msaada wa chakula katika kambi ya wakimbizi wa ndani (IDP) huko Agari, Kordofan Kusini, Juni 17, 2024. (Picha na GUY PETERSON / AFP)
Raia wakipanga foleni ili kujiandikisha kwa ajili ya utoaji wa msaada wa chakula katika kambi ya wakimbizi wa ndani (IDP) huko Agari, Kordofan Kusini, Juni 17, 2024. (Picha na GUY PETERSON / AFP) © GUY PETERSON / AFP

Mwezi Juni, kamati maalumu ya umoja wa Mataifa inayofuatilia mwenendo wa upatikanaji wa chakula duniani, ilisema watu zaidi ya laki 7 nchini humo wanakabiliwa na baa la njaa na kwamba kunahitajika udharura wa kushughulikia mzozo unaoendelea.

Tayari mashirika kadhaa ya kibinadamu ya umoja wa Mataifa na yale washirika, wametangaza njaa kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi ya Zamzam, ambako wapiganaji wa RSF wanaendeleza mashambulio.

Raia wa Sudan wakiwa kwenye foleni tayari kupokea chakula cha msaada.
Raia wa Sudan wakiwa kwenye foleni tayari kupokea chakula cha msaada. REUTERS – JOK SOLOMUN

Juma lililopita, umoja wa mataifa kupitia ofisi yake ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, ulisema licha ya kufanikiwa kufikisha misaada katika baadhi ya maeneo ambako raia wanahitaji msaada wa dharura, kulihitajika juhudi za ziada kuwafikia watu mamilioni ya raia ambao wanaendelea kukimbia machafuko.

Raia wa Sudan, waliofurushwa kutoka mji wa Sinjah, wakiwa kwenye foleni tayari kupokea chakula cha msaada August 22, 2024.
Raia wa Sudan, waliofurushwa kutoka mji wa Sinjah, wakiwa kwenye foleni tayari kupokea chakula cha msaada August 22, 2024. AFP – EBRAHIM HAMID

Haya yanajiri wakati huu ambapo jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF, wote hawaoneshi nia wala utayari wa kuzungumza kwa uwazi ili kumaliza vita na kupata suluhu ya mzozo wa kisiasa unaoendelea licha ya shinikizo toka jumuiya ya kimataifa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment