Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Urusi inakusudia “kuchukuliwa kwa uzito” baada ya kurusha kombora mpya zito la Orechnik huko Ukraine mwishoni mwa mwezi Novemba na kuonya kwamba iko tayari kutumia “njia zote” kujilinda, kulingana na matamshi yaliyotolewa siku ya Alhamisi na waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov.

Marekani na washirika wake lazima “waelewe kwamba tutakuwa tayari kutumia njia zote kuwazuia kufikia kile wanachoita kushindwa kwa kimkakati kwa Urusi,” amemwambia mwandishi wa wahariri na mtangazaji mwenye utata Tucker Carlson, ambaye alikuwa mwandishi wa kwanza wa Marekani kumhoji Vladimir Putin baada ya madhambulizi nchini Ukraine.
“Tunatuma ishara na tunatumai kuwa ya shambulio la mwisho, wiki mbili zilizopita (urushaji wa kombora) lilichukuliwa kwa uzito,” amesema waziri.
Kulingana na mamlaka ya Urusi, urushaji wa kombora hili lilitokana na milipuko iliyofanywa na Kyiv nchini Urusi kwa kutumia makombora ya Marekani na Uingereza.
Huku akisisitiza kuwa Urusi inataka “kuepusha kutoelewana” na Washington na washirika wake, Bw. Lavrov ameonya kwamba Urusi itatuma “ujumbe mpya ikiwa Marekani haitatoa hitimisho muhimu.”
“Tungependa kuwa na uhusiano wa kawaida na majirani zetu wote (…) na nchi zote na hasa nchi kubwa kama Marekani”, pia amebainisha Bw. Lavrov chini ya miezi miwili kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule Donald Trump huku utawala wa Joe Biden ukisema unataka “kuhakikisha kwamba Ukraine ina uwezo inaohitaji kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi.”
Bw. Lavrov ameshutumu utawala wa Biden kwa kuzidisha mzozo nchini Ukraine na hivyo “kuuwachia utawala wa Trump kama urithi mbaya.”
“Hatuoni ni kwa nini Urusi na Marekani hazikuweza kushirikiana kwa manufaa ya ulimwengu,” Lavrov amesema.
– “Vita vya mseto” –
“Rasmi hatuko vitani, lakini kile kinachotokea Ukraine, wengine wanakiita vita vya mseto, naweza pia kuiita vita vya mseto,” amesema, na kuongeza: “Ni dhahiri kwamba “Waukraine hawangeweza kufanya wanachofanya kwa silaha za kisasa za masafa marefu bila ushiriki wa moja kwa moja wa jeshi la Marekani.”
Bw Putin amesema kombora hilo la Orechnik liliruka kwa kasi mara kumi ya kasi ya sauti na halikuweza kunaswa na ulinzi wa anga. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelitaja shambulio hilo kuwa “pambano la hivi punde la wazimu wa Urusi.”
Akionya kwamba Moscow ilikuwa “tayari kwa hali yoyote”, Bw Lavrov hata hivyo amesisitiza kwamba Urusi “inapendelea zaidi suluhisho la amani kupitia mazungumzo kwa misingi ya kuheshimu maslahi halali ya Urusi”.
Akijadili jinsi makubaliano hayo ya amani yanaweza kuonekana, waziri Lavrov amesema Kyiv inapaswa, miongoni mwa mambo mengine, kukubali udhibiti wa Urusi wa “mikoa ya Donetsk, Kherson, Lugansk na Zaporizhia.”
“Mikoa hii sasa ni sehemu ya Shirikisho la Urusi, kwa mujibu wa Katiba, na hii ni ukweli,” amesema.
Bw. Lavrov pia amezungumzia kuwasili kwa Bw. Trump mamlakani, akimtaja rais mteule kuwa “mtu mwenye nguvu sana, anayetaka matokeo, asiyependa kuchelewesha jambo lolote.”
Donald Trump, ambaye anaingia madarakani mwezi Januari, ameahidi kumaliza vita haraka bila kueleza jinsi atakavyofanya.
Pia akihutubia Mashariki ya Kati, Bw. Lavrov ameelezea mashambulizi ya Israel huko Gaza kama “adhabu ya pamoja” kwa Wapalestina, iliyo “kinyume cha sheria za kimataifa za kibinadamu”.
Waziri huyo pia ametangaza kuwa “ana wasiwasi sana” na hali ya Syria ambapo makundi ya waasi yameteka maeneo yote ya ardhi kutoka kwa serikali ya Bashar Al Assad, mshirika wa Urusi. Amesema anapanga kuzungumza na maafisa wa Uturuki na Iran kuhusu hali hiyo siku ya Ijumaa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.