Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna wakati Mungu atatumia HILA za maadui zako kukupandisha zaidi.
Yaani, wewe sio wa kwanza, katika historia wapo wengi ambao walipandishwa kwa njia hii.
Wapo watu ambao leo wamekufukuza mahali wakiamini ndio mwisho wako.
Wasichojua kwa kufanya hivyo, wamekutengenezea fursa ya kupata nafasi kubwa zaidi.
Wengine wanakutengenezea uzushi wakiwa na dhamira ya kuharibu sifa yako.
Walichojua ni kuwa, hicho wanachofanya ndio kinawafanya watu watafute ukweli zaidi kuhusu wewe na wanayajua mema yako zaidi.
Ndio maana unahitaji uvumilivu kwenye maisha, kwa sababu lile wanalopanga wanadamu liwe madhara na anguko kwako, Mungu anaweza kulitumia kama njia ya KUKUINUA.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.