Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Kamanda wa kikosi maalum cha Korea Kusini, Kwak Jong-geun, amedai, siku ya Ijumaa, Desemba 6, kupokea amri kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ya “kuwatoa nje wajumbe wa Bunge la taifa” wakati ilipotangazwa sheria ya kijeshi usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, linaandika shirika la habari la AFP.
“Nilipokea maagizo kutoka kwa waziri wa zamani kuwaondoa wajumbe wa Bunge la taifa,” amesema wakati wa mahojiano na mbunge wa upinzani Kim Byung-joo, iliyorushwa kwenye YouTube.
Wakati huo huo mkuu wa chama tawala nchini Korea Kusini amesema Rais Yoon Suk Yeol wa nchi hiyo anaweza kuwaingiza raia kwenye hatari kubwa endapo hakutimuliwa.
Han Dong-hoon anayeongoza chama cha People Power, amesema ikiwa Rais Yoon ataendelea kubakia madarakani, huenda hatua kali kama vile sheria ya matumizi ya nguvu za kijeshi, zinaweza kurejea, na hivyo kuiweka Jamhuri ya Korea na raia wake hatarini.
Mkuu huyo wa chama tawala amesema pia kwamba lazima madaraka ya kikatiba ya Rais Yoon yasimamishwe.
Hata hivyo Han amesema Rais Yoon alikuwa ameagiza kukamatwa kwa wanasiasa wakubwa kwa madai kwamba wanapinga serikali.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.