Afrika Kusini: Miili sita yatolewa ndani ya mgodi uliozingirwa na polisi kwa wiki kadhaa.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Miili sita imetolewa ndani ya siku mbili kutoka kwa mgodi wa Stilfontein nchini Afrika Kusini ambapo mamia ya wachimbaji haramu bado wanaaminika kuwa chini ya ardhi. Kisima hiki cha dhahabu, kilomita 150 kusini magharibi mwa Johannesburg, kimezingirwa kwa wiki nne na vikosi vya usalama vya Afrika Kusini vilivyoazimia kuondoa watu hawa wanaoitwa “zama zama”.

Muonekano wa angani unaoonyesha shimo la mgodi lililo wazi huko Stilfontein, Novemba 17, 2024.
Muonekano wa angani unaoonyesha shimo la mgodi lililo wazi huko Stilfontein, Novemba 17, 2024. AFP – –

Nchini Afrika Kusini, polisi inaendelea kuzuia mgodi huu wa Stilfontein ambao haujatumika. Kwa wiki kadhaa, vikosi vya usalama vimekuwa vikizunguka kisima hiki cha dhahabu, kilichoko katika jimbo la Kaskazini Magharibi, kilomita 150 kusini magharibi mwa Johannesburg.

Kisima ambamo wachimbaji mia kadhaa wamejificha. Upatikanaji wa maji na chakula ni mdogo mno kwa wachimba migodi hawa haramu – wanaoitwa “zama zama” nchini Afrika Kusini – ambao wengi wao ni wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.

Katika siku mbili zilizopita, maiti sita zilitolewa katika mgodi huo. Miili miwili ilipatikana mnamo Desemba 3, mingine minne mnamo Desemba 4, kulingana na msemaji wa kitongoji cha Khuma, kilicho karibu na mgodi wa Stilfontein.

Wachimba migodi wengi waliokwama chini ya ardhi kwa karibu mwezi mmoja wanaishi katika jumuiya hii na familia zao zinazozidi kuwa na wasiwasi.

Wakazi wanajaribu wawezavyo kuwasaidia, licha ya kizuizi kigumu sana kutoka kwa polisi, ambao wanazunguka mgodi huo kulazimisha watu hawa kujisalimisha.

Mahakama yaidhinisha msaada wa dharura kufikia wachimbaji hao haramu

Mwishoni mwa mwezi wa Novemba, mahakama ya Afrika Kusini iliamua kwamba operesheni hii sio kinyume na katiba. Lakini kutokana na kuzorota kwa kasi kwa hali ya afya kwenye eneo la tukioi, Mahakama Kuu ya Gauteng hatimaye iliidhinisha mnamo Desemba 1 kwamba msaada wa dharura uwafikie wachimbaji madini.

Isipokuwa kwamba, kulingana na shirika la ndani ambalo lilifikisha malalamiko yake tena mbele ya mahakama wiki hii, polisi wanasita kuheshimu agizo hili, hata kama uhai wa watu hawa uko hatarini. Wengi wa wanaume hawa tayari ni wadhaifu sana kupanda juu kuelekea kutoka mgodini.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment