Sudan Kusini: Mazungumzo ya amani yarejelewa tena jijini Nairobi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Baada ya miezi minne na kufutwa kazi kwa ujumbe wa serikali, mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yaliyokwama yameanza tena jijini Nairobi, Kenya, ikiwa ni juhudi za hivi punde kujaribu mzozo wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu na ambao umedumaza uchumi wa nchi hiyo.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (kushoto) akisalimiana na  Pagan Amum, Mei 9, 2024 in Nairobi, Kenya.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (kushoto) akisalimiana na Pagan Amum, Mei 9, 2024 in Nairobi, Kenya. © Brian Inganga / AP

Mazungumzo haya yanafanyika kati ya serikali ya Juba na makundi ya upinzani ambayo hayakuwa sehemu ya makubaliano ya mwaka 2018 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Juhudi za kumaliza mzozo huu zilikwama baada ya Rais Salva Kiir kuwafuta kazi wajumbe wa serikali waliokuwa wakishiriki na timu mpya kuteuliwa kuwakilisha serikali, lakini walishindwa kusafiri hadi Nairobi mara mbili.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir - Nairobi 11 Mei 2014.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir – Nairobi 11 Mei 2014. REUTERS/Thomas Mukoya

Mwezi jana, Kiir alisema mazungumzo ya Nairobi hayakukusudiwa kubadilisha makubaliano ya 2018, bali kushughulikia wasiwasi wa makundi yaliyosalia nje ya makubaliano hayo.

Wakati makubaliano ya 2018 bado hayajatekelezwa kikamilifu, Sudan Kusini imeahirisha uchaguzi hadi 2026 kutokana na matatizo ya usajili wa wapigakura na mzozo wa kiuchumi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment