Kabla ya haujatumia pesa,Maswali 5 Ya Kujiuliza .

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Kitu hiki kilikuwa kwenye bajeti yangu?

ii. Kwa nini nataka kununua/kuwa nacho (Motive)?

iii. Ni lazima nitumie sasa hivi?

iv. Nimetafuta kulinganisha bei?

v. Matumizi ninayofanya yako kwenye kundi gani?

Katika Makala Hii Tutazungumzia Swali la Tano

– Matumizi ninayofanya yako kwenye kundi gani?

Pesa yoyote unayoitoa ni vizuri kujua inaenda kwenye kundi gani la matumizi yako.

Kama bado unahangaika na kujua hili tafadhali usisahau kutafuta kitabu cha MONEY FORMULA (Elimu Ya Fedha Isiyofundiswa Shuleni) na ONGEZA KIPATO CHAKO (Maarifa Juu Ya Fedha, Biashara na Uwekezaji), vitakusaidia sana.

Ni lazima ujifunze kutumia pesa yako kimkakati, yaani uamue kuwa inaenda wapi na inaenda kufanya nini.

Hii itakusaidia kutotumia pesa ambayo inatakiwa kwenda kwenye uwekezaji ikaishia kwenye kujiburudisha.

Kumbuka kwenye makundi ya matumizi yako, utagundua kuwa yako yale ambayo ukitumia pesa ndio inapoteza kabisa.

Nyingine inaenda kukaa na utaikuta ilivyo na nyingine inaenda kuzaa na itakupa zaidi ya uliyoweka.

Kila wakati kabla haujatumia jiulize, hii ninayotoa inatoka kama kundi gani?

Kama unataka Kujifunza Mbinu za Kuhakikisha Haupotezi PESA, LEO nashauri usome eBook yangu ya “NIDHAMU YA PESA”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment