Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Siku moja tajiri mmoja alienda baharini (Beach) kupunga upepo.
Wakati akitembea huku na kule akiwaza na kuwazua juu ya biashara zake, mara ghafla akamwona mvuvi mmoja amekula zake tano

(amelala chali na kuota jua) na mtumbwi wake pembeni imejaa samaki.
Tajiri akamsogelea na kumwambia……
Tajiri: Wewe Mbona unalala SASA hivi, amka ukavue samaki, uuze ili upate hela?
Mvuvi: Ili iweje?
Tajiri: Uwe na pesa nyingi uajiri watu wakusaidie kuvua samaki.
Mvuvi: Ili iweje?
Tajiri: Biashara YAKO iwe kubwa na uwe ununue meli uanze kusafirisha nje ya nchi.
Mvuvi: Ili iweje?
Tajiri: Uwe na hela nyingi, uwe unakuja tu bahari kupumzika na kupunga upepo kama Mimi.
Mvuvi: Kwani hapa nafanyaje?
Umejifunza nini kwa Tajiri na Mvuvi?
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.