Afrika: Nchi zinazoendelea zilitumia Dolla Trilioni 1.4 kulipa madeni: Beni ya Dunia.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Benki ya Dunia imesema nchi zinazoendelea zilitumia dola trilioni 1.4 kuhudumia madeni yao ya nje mwaka 2023 huku gharama za riba zikipanda hadi kiwango cha juu katika kipindi cha miaka 20, hali iliyozifanya nchi hizo kubana bajeti ya mahitaji katika sekta muhimu za afya, elimu na mazingira.

Nembo ya benki kuu ya dunia.
Nembo ya benki kuu ya dunia. © reuters

Katika ripoti yake mpya kuhusu madeni, inaonesha kuwa kiujumla malipo ya riba kwa madeni ya nje kwa mataifa yanayoendelea yaliongezeka hadi kufikia dola za marekani bilioni 406.

Benki ya dunia imeongeza kuwa, Ingawa ulipaji ulipungua kwa karibu asilimia 8 hadi kufikia dola bilioni 61.6, gharama za riba zilipanda kwa kiwango cha juu na kufikia dola bilioni 34.6 mwaka 2023, ikiwa ni mara nne ya kiasi cha miaka kumi iliyopita.

Aidha ripoti inasema kwa wastani, nchi zinazostahiki kupewa mkopo zinatumia wastani wa asilimia 6 ya mapato ya mauzo ya nje kuhudumia madeni ya nje, kiwango ambacho hakijaonekana tangu 1999.

Benki ya Dunia inasema kuwa hadi mwishoni mwa mwaka 2023, deni la nje linalodaiwa na nchi zote za kipato cha chini na kati lilifikia rekodi ya dola trilioni 8.8.

Kubanwa na madeni kwa nchi maskini kumezilazimisha kugeukia taasisi za kimataifa, kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, ambapo zimeshatoa dola bilioni 51 kuanzia mwaka 2022 na 2023.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment