Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Malengo yangu hayajatimia mwaka huu licha ya kutumia Nguvu, muda na rasilimali nyingi. Je, niyachane chane nitupe kwenye “Dustbin” mwakani nianze upya?
Watu wengi tunajiuliza hili swali SASA hivi…..!!!
HAPANA!
Haimanishi kile ulichokianzisha mwaka huu, kwa vile hakijatimia au hakijaleta matokeo Kwa haraka ndiyo uache kabisa na kutafuta kitu kingine mwakani 2023.
Hata kama hakijatimia, usitupe malengo au Ndoto yako. Kuna mazao yanahitaji zaidi ya kumwaka Kuvunwa. Endelea kupalilia.
Kikubwa mwakani unaanzia ‘Somewhere’ siyo sifuri.
Kuna watu kila mwaka MPYA wanaanza UPYA katika KILA JAMBO.
Ndiyo, mwaka MPYA na mambo MAPYA. LAKINI, haimanishi kila mwaka Wewe unanzisha hiki mara kile, alafu kinakufa hata Kabla mwaka haujaisha.
Mwaka unaofuata unaanzisha tena kitu kingine.
Moja kitu nilichokifunza kwenye maisha ni kwamba, kwenye eneo la “GOAL SETTING” kuna malengo ambayo ni MALENGO MAMA, yaani “LIFE TIME GOALS”.
Ni MALENGO ambayo ije jua, ije Mvua ni lazima upambane kuyafikia. Yaani, mabadiliko ya mwaka na majira HUONGEZA NGAZI au HUONYESHA UELEKEO mpya LAKINI, LENGO (TARGET) iko pale pale.
Ni MALENGO ambayo yanahitaji uyape muda ili upate matokeo.
Mara nyingi mchakato wake ni MGUMU LAKINI MATOKEO yake ni Makubwa.
Usiyakatie tamaa, MALENGO YAKO kisa Tu mwaka huu mambo hayajakuendea vizuri.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.