DRC: Viongozi wa kijadi wanataka kuhusishwa katika mchakato wa amani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Viongozi wa kijadi na wale kutoka makabila mbalimbali katika mikoa ya Kivu kaskazini, Kusini na Maniema Mashariki mwa DRC, sasa wanataka wahusishwe katika mchakato wa kutafuta amani mashariki mwa nchi hiyo.

Mazungumzo ya kupata suluhu kuhusu utovu wa usalama mashariki ya DRC yamekuwa yakiongozwa na waptanishi kutoka Angola.
Mazungumzo ya kupata suluhu kuhusu utovu wa usalama mashariki ya DRC yamekuwa yakiongozwa na waptanishi kutoka Angola. © ALEXIS HUGUET / AFP

Baada ya mkutano wa siku tatu Jijini Goma, katika juhudi za kuhimarisha amani na usalama DRC, ndipo viongozi hao wa asili kutoka mashariki mwa Congo Kivu kusini, Kivu kaskazini na Maniema, walielezea malalamiko na masikitiko yao wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Goma.

Joseph Nkinzo ni mwakilishi wa viongozi hao wa asili mashariki mwa Congo

‘‘Viongozi wa serikali waitisha watu Kinshasa kuzungumza Kuhusu amani, tumeona kwamba mazungumzo haya yote haifanye viongozi wa makabila hawahusishwe sana kwa kutafuta amani ndani ya nchi mashariki ya Congo.’’ alisema Joseph Nkinzo.

Viongozi hao wanataka kujumuishwa katika mchakato kwa kupatikana kwa amani mashariki mwa DRC.
Viongozi hao wanataka kujumuishwa katika mchakato kwa kupatikana kwa amani mashariki mwa DRC. © Tshube Ngorombi RFI

Viongozi hao wamelalamikia pia kuwepo kwa mikataba mingi nchini DRC.

‘‘Tumeomba kwamba mkataba wa Abdis Ababa uliosainiwa 2013 pamoja na huu mkataba wa sasa unaoelekea kusainiwa hapo Luanda, hizi mbili ziwekwe pamoja ili tusiwe na mikataba kadhaa ambayo inaweza tuweka kwa shida.’’ alieleza Joseph Nkinzo.

Nao viongozi wa serikali katika maeneo yanayokabiliwa na ukosefu wa salama wamekuwa na kauli hii.  Kibira Isaac ni mmoja wao.

‘‘Basi Serikali ya Congo inaweza kusikiliza hilo ombi ili wote washirikishwe maana amani si ya mtu mmoja, demokrasia inataka kushirikisha watu wote ambao wanaweza kuleta amani.’’ Alisema Kibira Isaac.

Serikali ya DRC na washirika wake imekuwa ikipambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC.
Serikali ya DRC na washirika wake imekuwa ikipambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC. AFP – GLODY MURHABAZI

Haya yanajiri wakati huu kundi la M23 likiendela kushutuliwa kuvidhibiti vijiji kadhaa, likisababisha maelfu ya raia kuhama makazi yao mashariki mwa Congo DRC.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment