Crab Mentality ni hatari sana.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja kati ya njia rahisi ya kuwakamata Kaa kwa ajili ya kitoweo, ni kwa kutumia “BOKSI au NDOO” iliyo wazi kwa juu.

Ambapo Kaa huanza kuingia mmoja mmoja mpka boksi/ndoo inajaa kisha hufunikwa.

Swali ni je, kama boksi/ndoo iko wazi kwanini Kaa hawawezi tena kutoka na kuepuka kukamatwa?

Kaa angeweza kirahisi kutoka nje ya ndoo/boksi, lakini kitu kinachomkwamisha ni akili za “KAA WENZAKE”.

Yaani, wakati Kaa mmoja anapojaribu kujikokota ili kutoka nje ya ndoo/boksi, Kaa wengine HUMVUTA kwa makucha yao na kumrudisha ndani ndoo/boksi.

Mwishowe hakuna anayetoka, wote huishia kukamatwa baada ya ndoo/boksi kufunikwa. _________________________

Katika maisha yetu ya kila siku watu wenye akili/mawazo kama ya KAA tupo wengi sana.

Umeshawahi kusikia kauli ya, ” BORA TUKOSE WOTE”.

Yaani inatokea deal au fursa ambayo MTU fulani katikati yenu anaimudu vizuri, lakini anawekewa VIKWAZO na VIPINGAMIZI ili tu asipate nafasi ya kuchukua fursa hiyo.

Hao ni watu wenye “Crab mentality”.

Kila mahali katika maisha yetu, aidha makazini, kwenye biashara, mashuleni n.k……

….. Watu wenye ” Crab mentality ” wako wengi sana.

Hivyo ni muhimu kwanza Mimi na wewe tuwe wa kwanza kubadilisha mitazamo na mawazo yetu juu ya wengine.

Kwamba, inapotokea nafasi/fursa ambayo hatuna uwezo nayo, lakini kuna MTU mwingine anaweza, tumwachie nafasi.

KWANI, akifanikiwa anaweza hata ikawa faida kwa wengine kwa namna moja au nyingine.

Ushawahi kukutana na watu wa namna hii.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment