Ziara ya rais wa Gabon mjini Brussels, ishara ya kuimarisha uhusiano na EU

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa mpito wa Gabon, Brice Oligui Nguema, ametembelea taasisi za Umoja wa Ulaya (EU) mjini Brussels. Katika orodha ya ziara hii ya kikazi, ushirikiano kati ya Gabon na EU, masuala ya amani na usalama, maendeleo endelevu pamoja na mseto wa kiuchumi na kimazingira, ambayo inasisitiza uimarishaji wa uhusiano kati ya EU na Gabon.

Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema mjini Paris mnamo Julai 25, 2024.
Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema mjini Paris mnamo Julai 25, 2024. © Ludovic Marin / AFP

Wakati muhimu wa ziara ya rais wa mpito wa Gabon huko Brussels ulikuwa mkutano wa kazi na mabadilishano ya kisiasa na idara ya Utekelezaji ya Nje ya Ulaya, diplomasia ya EU na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel ambaye alimwalika Brice Oligui Nguema.

Umoja wa Ulaya unasema ushirikiano na Gabon katika kipindi hiki cha mpito ni mojawapo ya mafanikio ya sera ya Afrika ya Umoja wa Ulaya (EU). Brice Oligui Nguema amewahakikishia Wazungu kuhusu nia yake ya “kuheshimu ahadi zake za kimataifa”.

Marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi pamoja na uanzishwaji wa daftari la uchaguzi pia yamekuwa miongoni mwa mijadala yao, pamoja na kuboresha uchumi wa Gabon hasa, reli, barabara na shule.

Kuelekea mpito wa kuigwa?

Kwa Umoja wa Ulaya, Gabon si nchi kama nyingine yoyote, ni “mpito wa kupigiwa mfano kwa bara la Afrika” kulingana na afisa wa Ulaya ambaye anatoa tathmini ya mkutano huu. Anasema kuwa rais wa Gabon ameiomba EU kutuma ujumbe wa wachunguzi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka ujao, ombi ambalo linaweza kupokelewa vyema, kwani Wazungu wanaonekana kutaka kuonyesha “uungaji mkono mkubwa wa kisiasa” – haswa baada ya kurejea kwa wataalam wa EU, ambao waliidhinisha kuendeshwa kwa kura ya maoni mnamo Novemba 16.

Wakati wa mapinduzi ya 2023 dhidi ya Ali Bongo, mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell alibaini, badala yake kwamba haikuwa mapinduzi ya kawaida na wakati wa kutoa nafasi kwa timu mpya kuwa mkuu wa taasisi za EU, viongozi wa Ulaya wanaomaliza muda wao wanafuraha kumaliza mamlaka yao kwa “maelezo chanya” katika uhusiano wao na Afrika.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment