Mambo yanapoanza kama mwiba.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mambo mengi ambayo yamegeuka kuwa MWIBA kwenye maisha Yetu, ni Yale ambayo yalianza huku tunayaona.

Kuna hatua kama 3 ambazo huwa yanapitia:

Kwanza huwa ni changamoto ya kawaida. Hii huonekana kwanza kama ni kitu tunachoweza kukimudu/kukificha na tukakishinda.

Mara nyingi tunakipuuzia na kuona kwamba hakitakuwa na madhara Kwenye maisha yetu. Hapo ndipo kinaingia hatua ya pili na kugeuka kuwa ni TATIZO (PROBLEM).

Likifika hatua hii huwa linaanza kukusumbua na kukukosesha RAHA. Hapa huwa linaanza kukupa na “stress” na unaanza kuona linakusumbua.

Usipolishughulikia Kwenye hatua hii, litageuka na kuanza kuwa ni DHARUA (Emergency). Likishafika hatua hii, mara nyingi utalazimika/kulazimishwa kufanya maamuzi au kuchagua USICHOKIPENDA.

Hekima ni kukabiliana na tatizo likiwa halijafika mbali sana. Usilifunike. Shughulika nalo leo ili Usitumie GHARAMA kubwa KESHO.

Kama umeipenda makala hii…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment