Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), karibu robo ya wakazi, au zaidi ya watu milioni 25, wanakabiliwa na njaa, ikiwa ni pamoja na milioni tatu wakiwa katika ali ya dharura za kibinadamu. Ili kukabiliana na mgogoro huu, FAO (Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa) linakadiria kuwa linahitaji dola milioni 330. Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Beth Bechdol, amezuru mashariki mwa nchi, ambapo amekutana na watu waliokimbia makazi yao.

Kwa mujibu wa FAO, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeorodheshwa miongoni mwa nchi zilizo katika hatari kubwa ya njaa na inaweza kukumbwa na njaa hiyo iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa. Beth Bechdol, naibu mkuŕugenzi mkuu wa shiŕika hilo, anasema ni muhimu kuwekeza zaidi katika kilimo: “Lazima tuzingatie kujenga mazingiŕa ya amani katika eneo la mashaŕiki mwa nchi. Tunajua kwamba migogoro katika eneo hili ndiyo chanzo cha watu kuhama. Kuna matatizo makubwa ya chakula katika kambi za wakimbizi wa ndani. Amani ni jambo la kwanza kubadilisha hali hii. Lakini shida ya ufadhili ni nadra kuzingatiwa. “
Kutokana na changamoto hizi, FAO imetekeleza miradi kadhaa ya dharura ili kukidhi mahitaji ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro katika mikoa ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Aristide Ongone Obame, mwakilishi wa shirika hilo nchini DRC, anaeleza: “Kwa sasa tunaingilia kati kambi za wakimbizi wa ndani ili kuwapa kile tunachokiita msaada wa dharura wa kilimo. Hii inawawezesha kuzalisha wenyewe badala ya kuishi kwa msaada wa chakula pekee, jambo ambalo halitoshi. Pia tunatoa wanyama wadogo kwa mifugo hali ambayo hutoa matokeo haraka sana. “
Kulingana na uchambuzi wa hivi punde wa usalama wa chakula, uliochapishwa mwezi Oktoba, zaidi ya watu milioni 25 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini DRC.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.