Bunge la Ulaya: Timu mpya ya von der Leyen yaidhinishwa Strasbourg

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bunge la Ulaya huko Strasbourg siku ya Jumatano, Novemba 27, limeidhinisha timu mpya ya Tume ya Ulaya, ambayo itachukua madaraka mwanzoni mwa mwezi Desemba 2024 katikati ya hali ya msukosuko mkubwa wa kiuchumi na kijiografia.

Bi Ursula von der Leyen (kushoto), Rais wa Tume, na Bi Roberta Metsola (kulia), Spika wa Bunge la Ulaya, katika Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Novemba 27, 2024.
Bi Ursula von der Leyen (kushoto), Rais wa Tume, na Bi Roberta Metsola (kulia), Spika wa Bunge la Ulaya, katika Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Novemba 27, 2024. AFP – FREDERICK FLORIN

Mnamo Novemba 27 huko Strasbourg, serikali mpya ya Umoja wa Ulaya imepata kura 370 dhidi ya 282 ambazo zilipinga na 36 hawakupiga kura). Muhula wa pili wa Ursula von der Leyen utaweza kuanza, takriban siku hamsini kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump kama rais wa Marekani. Ni hisia ya uharaka ambayo imetawala katika taasisi za Ulaya. Ulaya “haina muda wa kupoteza” ameonya Ursula von der Leyen, Rais wa Tume, akiweka kipaumbele kwa ushindani “kuziba” pengo na Marekani na China.

“Uhuru wetu hutegemea zaidi kuliko hapo awali nguvu zetu za kiuchumi,” amebainisha. Kwa upande wa ulinzi, Ursula von der Leyen amesisitiza juu ya haja ya kufanya zaidi kushindana na matumizi ya kijeshi ya Urusi, wakati kurejea kwa Donald Trump kunazua hofu ya kujitenga kwa Marekani nchini Ukraine. “Gharama zetu lazima ziongezeke,” amesema Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 66. “Urusi inatumia hadi 9% ya Pato la Taifa kwa ulinzi. Ulaya hutumia wastani wa 1.9. Kuna kasoro katika mlingano huu,” pia anabainisha.

“Njia mbili”

Kujitayarisha kurejea kwa Bw. Trump ni “changamoto ya dharura zaidi” kwa Umoja wa Ulaya, EU, anasema Luigi Scazzieri, mchambuzi katika Kituo cha Mageuzi ya Ulaya. Kwenye “mambo mawili”: biashara, na ahadi ya rais mteule kutoka chama cha Republican ya kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za Ulaya, na “usalama”, na vita huko Ukraine. Licha ya changamoto hizi kuu, Bunge la Ulaya litakuwa limejitahidi kabla ya kuidhinisha Tume mpya.

Makundi hayo yaligombana kuhusu makamu wa rais aliyopewa Muitaliano Raffaele Fitto, mwanachama wa chama cha mrengo wa kulia cha Giorgia Meloni cha Fratelli d’Italia, huku upande wa kushoto ukidai kudumishwa kwa “afya”. Von der Leyen alichukua nafasi hii ya makamu wa rais, ambayo inamuwezesha kudumisha uhusiano wake na Bi. Meloni. “Ni chaguo ambalo nilifanya,” amesema mbele ya wabunge wa Umoja wa Ulaya.

Siku kadhaa za mvutano

Baada ya siku kadhaa za mvutano, EPP (kulia), watetezi wa Renew na wanademokrasia wa kijamii waliishia kutia muhuri makubaliano ya kuidhinisha makamishna wote waliopendekezwa, kwa mara ya kwanza katika miaka ishirini. Miongoni mwa sura mpya: Waziri Mkuu wa zamani wa Estonia, Kaja Kallas anakuwa mkuu mpya wa diplomasia ya Umoja wa Ulaya, mwanasiasa wa Ufaransa Stéphane Séjourné anachukuwa nafasi ya makamu wa rais mwenye jalada pana la mkakati wa viwanda, na mwanasoshalisti wa Uhispania Teresa Ribera atakuwa makamu wa rais wa mpito wa kiikolojia na ushindani. Tume hii mpya inaegemea upande wa kulia ikiwa na karibu nyadhifa kumi na tano, kati ya 27, zilizotengwa kwa EPP (kulia), nguvu kuu ya kisiasa Bungeni.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment