Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika Jumatano hii, Novemba 27 kote nchini Tanzania. Kwa jumla, zaidi ya vijiji na vitongoji 75,000 vitachagua wawakilishi wao wa mitaa kwa kipindi cha miaka mitano. Uchaguzi ambao unafanyika baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya kisiasa nchini na kutoweka kwa wapinzani wa kisiasa, na mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa rais.

“Njooni kwa wingi”, ni kichwa cha habari cha Gazeti la Daily News wakati uchaguzi wa serikali za mitaa wa Jumatano, Novemba 27 hauonekani kusisimua umati wa watu nchini Tanzania. Hata hivyo chama tawala cha CCM, kinadai kuwa asilimia 95 ya wananchi wamejiandikisha kupiga kura. Kielelezo kinachoacha baadhi ya vyombo vya habari huru kuwa na shaka. Badala yake, wananyooshea kidole serikali kuinilia katika uchaguzi huu.
Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametangaza kwa upande wake kuwa karibu asilimia 70 ya wagombea wake walienguliwa, mara nyingi kwa sababu za kiutawala kama vile fomu kutokamilika vizuri au kukosa mihuri. Katika wiki za hivi karibuni, baadhi ya wapinzani wa kisiasa wamepigwa marufuku na polisi kufanya kampeni , au hata kukamatwa.
Hata viongozi wa kidini, wanaoheshimika sana nchini, wameingilia mjadala huo. Mchungaji Wolfgang Pisa, Mkuu wa Kongamano la Maaskofu Tanzania, alikemea “upendeleo wa wazi” kwa wagombea wa CCM.
Chama cha Rais Samia Suluhu kilitabiri, hata kabla ya kura, “ushindi mkubwa” ujao. Mbinu zinazofanana na zile za aliyekuwa rais wa kimabavu John Magufuli, ambaye hata hivyo rais wa sasa aliahidi kutengana nazo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.