Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kila mtu ana KIPAJI, Lakini Siyo kila mtu anajua Kipaji chake au anaishi Kipaji chake.
Najua unawafahamu watu wenye vipaji vikubwa sana,….
LAKINI, mpaka leo hakuna chochote wanachokifanya kupitia vipaji.
Najua unatamani kuendeleza Kipaji Chako, tena kianze kukulipa hata kama ni kidogo Kidogo,…
LAKINI, bado umekwama. Hujui uanzie wapi kufanya nini Ufanikiwe.
Najua unawafahamu watu ambao unawatamani wafike mbali, tena viwango vya juu kupitia vipaji vyao,….
LAKINI, bado wamebaki pale pale, tena wengine wameshapotea kabisa.
Najua Kuna unatamani unatamani kutumia Kipaji chako ili kugusa maisha ya watu na kikupe matokeo,….
LAKINI, mpaka sasa hivi hujaanza kufanya lolote kwa sababu hujui pakuanzia.
YES!!! Ni ukweli kwamba kila mtu katika safari ya KUJITAFUTA hupitia katika hali hiyo…
Inaitwa, “BLINDNESS STAGE”…
Ni hali ambayo unakuwa kama huoni vile nini Cha Kufanya..
Unakuwa kama vile, Umekwama (STACKED),
Tena, Umekwama kwa sababu ambazo hazijulikani, (UNKNOWN REASONS).
Kila ukifanya au ukigusa hiki au kile kinachohusiana na KIPAJI chako, Hakisogei…
Mwishowe unabaki kuwa, “MR (S) TRIAL and ERROR”..Mzee wa Kubahatisha na Kujaribu.
Kipaji siyo kama kucheza, KAMARI, Hapana!!
Ni kitu ambacho kinahitaji mpango mkakati maalum wa kuendeleza au kukuza…
..”TALENT GROWTH STRATEGY”…
Kitu ambacho watu wengi Wanashindwa kuwa nayo!
HONESTLY!!
Hata Mimi mwanazoni, sikuwa nayo,
Kitu ambacho kilinigharimu Sana na kunifanya nichelewe kutumia Kipaji changu.
IMAGINE!! Tangu nikiwa Primary nilianza kunusa, harufu na kuanza kuhisi chembe chembe za Uandishi ndani yangu,
BUT, ilinichukua miaka zaidi ya 15 kuanza kukutumia…
Je, ni kweli nisingeweza kuanza kipindi hicho tangu nijue Nina Kipaji hicho?
HAPANA, ningeweza. Kuna watu wakiwa na miaka 5 tu, tayari washaanza.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.