Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Tukio hilo limetokea siku ya Jumapili, Novemba 24 karibu na ubalozi wa Israel mjini Amman, ambapo kijana mmoja aliwafyatulia risasi maafisa wa polisi wa Jordani.
Kijana mwenye umri wa miaka zaidi ya ishirini aliwafyatulia risasi maafisa wa polisi wa Jordani karibu na ubalozi wa Israel mjini Amman. Shambulio hilo lilipelekea maafisa wa polisi watatu kujeruhiwa. Mshambuliaji, mwenye umri wa miaka 24, aliuawa papo hapo.
Polisi wa Jordani hawajatoa taarifa kuhusu uwezekano wa kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi.
Kulingana na mtaalam wa usalama Omar Al-Raddad, inaonekana kwamba shambulio hilo lilikuwa kitendo cha kipekee, kisicho na uhusiano wowote na makundi yenye silaha: “Shambulio hili lina vipengele viwili: kunaweza kuwa na uhusiano na makundi ya wafuasi wa Hamas na Hezbollah, au kunaweza kuwa na sababu za kulipiza kisasi dhidi ya polisi. Lakini ni uchunguzi ambao utalazimika kubainisha sababu.”
Shambulio lililoelezewa kama la “kigaidi”
Msemaji wa serikali Mohammed Momani ameliita shambulizi hilo la “gaidi” na kuahidi kwamba waliohusika wataadhibiwa: “Hali ya afya ya maafisa wa polisi waliojeruhiwa katika shambulio hilo iko shwari, na tunatumai watapona haraka. Kama serikali, tunawaunga mkono kikamilifu, walipokuwa wakitekeleza wajibu wao wa kulinda usalama na utulivu wa Jordani.”
Kwa zaidi ya mwaka mmoja, maandamano yamekuwa yakifanyika karibu na ubalozi wa Israel, kuunga mkono Wapalestina na kupinga vita huko Gaza. Hakuna mfanyakazi hata mmoja katika ubalozi huo , baada ya Jordani kukataa kumruhusu mwanadiplomasia wa Israel kurudi Amman.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.