Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

1). Ukiona au ukisikia FURSA ambayo inawafaa Wana, WASHUTUE.
2). Kama Washikaji wanafanya biashara au Mishe ambazo unaweza kuwaungisha, WAUNGISHE.
3). Ukipata Connection mahali au sehemu ambayo inawafaa Wana, WAPATIE.
4). Ukiona washikaji wanahangaika kufanya kitu fulani, ambacho una uwezo wa kuwasaidia au unamjua mtu anweza kuwasaidia, FANYA HIVYO.
5). Ukiona Wana Wanafanya makosa Fulani fulani au wanafanya vitu ndivyo sivyo, WAAMBIE.
6). Ukiona Wana wamekwama kabisa, hawajui hili Wala lile, na unaweza kuwapa Mawazo ya kuwasaidia, WASHAURI.
7). Ukiona Wana wanakufuta uwasaidia kitu fulani au uwape Ushauri ambao uko ndani ya uwezo wako, WASIKILIZE.

. Ukiona Wana wanakaribia kukata tamaa, na neno lako linaweza kuwapa nguvu ya kusogea mbele kidogo, WATIE MOYO.
9). Ukiona Wana Wanakutafuta uwapate support kwenye mambo kadha wa kadha, na unaweza ukapata muda ya kujumuika nao, SHIRIKI (WAPE COMPANY).
10). Kama Wana Wanafanya vitu vizuri na wewe uko katika ‘Position’ nzuri ya kuwasemea Ili mambo yao yanyooke na kutengeneza Network kubwa, WASEMEE VIZURI.
11). Kama wana wamepambana sehemu au mahali kwa kumwaga jasho hadi tone la mwisho mpaka dili lao fulani likatiki, USIWARIBIE.
12). Kama uko katika nafasi fulani ya Juu, na chini Yako Kuna Wana Wanafanya kazi chini Yako, USIWASINICHI au KUWABANIA RIZIKI.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.