NATO: Mabalozi kutoka mataifa wanachama kukutana mjini Brussels

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

NATO na Ukraine zinatarajiwa kukutana wiki ijayo mjini Brussels, kikao kinachokuja baada ya Urusi kurusha silaha za masafa marefu zinazopingwa kutumika kwenye vita (inter-continental ballistic missile) kuelekea nchini Ukraine.

Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte.
Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte. AP – Omar Havana

Kikao hicho cha Jumanne ya wiki ijayo kimeitishwa na Kyiv baada ya mashambulio ya Urusi katika mji wa Dnipro ambapo ni mabalozi wa nchi wanachama wanaotarajiwa kuhudhuria.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Alhamis ya wiki alithibitisha kwamba Moscow ilikuwa imeishambulia Ukraine kwa kutumia kombora la kisasa ambalo alisema linauwezo wa kubeba silaha za nyukilia.

Rais wa Urusi anasema nchi yake itajibu dhidi ya mataifa yanayoiruhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu dhidi yake.
Rais wa Urusi anasema nchi yake itajibu dhidi ya mataifa yanayoiruhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu dhidi yake. © AP – Vyacheslav Prokofyev

Kwa mujibu wa msemaji wa NATO ,hatua ya Urusi haitobadili mkondo wa mzozo na haiwezi kuwazuia washirika wa Ukraine kuendelea kuisaidia.

Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Putin amesema nchi yake ilirusha kombora hilo kama njia moja ya kujibu hatua ya Ukraine kurusha kombora la masafa marefu kuelekea nchini mwake.

Wiki hii, Ukraine imeripotiwa kutekeleza mashambulio ya makombora ya masafa yaliotolewa na Marekani na Uingereza kuelekea Urusi.

Nchi wanachama NATO zimeahidi kuendelea kuisaidia Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.
Nchi wanachama NATO zimeahidi kuendelea kuisaidia Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi. © Omar Havana / AP

Aidha Putin ameeleza kwamba inauwezo wa kushambulia maeneo ya kijeshi katika mataifa yanayoiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu dhidi ya nchi yake.

Mwanchama mkuu wa NATO na mshirika wa Ukraine, nchi ya Marekani imeituhumu Urusi kwa kuzidisha mzozo wa Ukraine.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment