Pesa imejificha maeneo haya manne.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

MAENEO 4 Ya KUTENGENEZA PESA Kwa
Haraka Unapoanza KUJIAJIRI…

Kawaida pesa huwa inajificha:

i. Kwenye Mikono ya Watu
ii. Kwenye Matatizo
iii. Kwenye Bidhaa
iv. Kwenye Mawazo (Ideas)

Leo katika makala hii tutaangalia eneo la pili.

– Kwenye Matatizo

Sehemu ya pili ambayo pesa huwa inajificha ni kwenye matatizo ya watu.

Kila tatizo unaloliona kwenye maisha yako ni fursa ya kutengeneza pesa zaidi.

Unachotakiwa kuhakikisha ni kuwa unatatua matatizo ya watu wengi zaidi ili kutengeneza fedha nyingi zaidi.

Unapoanza kujiajiri jiulize:

Kuna tatizo gani ambalo nina uwezo wa kuwatatulia watu?

Kila biashara inayokuzunguka ambayo wewe huwa unalipa pesa ni kwa sababu kuna tatizo wanakutatulia.

Mwandishi mashuhuri duniani, Mchungaji na
mfanyabiashara mkubwa raia wa Marekani, T.D. Jakes katika kitabu chake cha…

…“Soar” anachoelezea jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara kutokea chini kabisa.

Kwenye kitabu hicho anasema namna nzuri ya kupata pesa zaidi ni kutafuta matatizo ambayo yanawagusa wengi zaidi (Juicy Problems).

Hebu jiulize leo tangu asubuhi umetumia pesa zako katika mambo gani?

Ukichunguza utagundua ni changamoto
ambazo wengine wameamua kuzitatua kwa niaba yako…

…na wewe unawalipa ili wakusaidie kuzitatua.

Unapolipa pesa ni kusema umeamua kuwaruhusu wengine watatue matatizo
kwa niaba yako kwa sababu hauna uwezo wa kuyatatua.

Ama unao uwezo lakini hauna muda wa kufanya hivyo.

Unachotakiwa kujua ni kuwa ili kutengeneza pesa ya uhakika unapoamua kujiajiri, hauwezi kutatua kila tatizo lililoko mbele yako.

Bali tafuta tatizo fulani mahususi/matatizo machache na uyatengenezee mkakati
wa kuanza kuyatatua kwa ufanisi mkubwa.

Jiulize: Muuza chakula anatatua tatizo gani?

Muuza nguo?

Mwenye daladala/bodaboda je?

Ukihitaji kujifunza kwa kina MAENEO 4 Ya KUTENGENEZA PESA Kwa Haraka Unapoanza KUJIAJIRI…

HATUA 6 ZA KUJIAJIRI, Jinsi Ya Kuingiza Kipato Kwa Kazi Yako Mwenyewe.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment