Utabadilisha mfumo au Utafwata nyayo.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna mama mmoja alikuwa anaishi na binti yake. Huyo mama kila akipika samaki, anakata katikati kabla kukaanga (chungu chake kilikuwa kidogo).

Basi binti yake akakariri kwamba, samaki kabla ya kupikwa anakatwa katikati. Alipoolewa, alinunuliwa chungu kikubwa zaidi ya ile ya mama yake.

LAKINI, kila alipopika samaki alikata katikati japo chungu kilikuwa kikubwa. Yeye hakuwahi kujiuliza au kumuuliza mama yake kwanini anakata katikati.

Siku moja mume wake akamuuliza, “Vipi mbona hawa samaki umewakata Kati na chombo kinatosha?”.

Akajibu, “Tangu nikiwa mdogo hivi ndivyo mama yangu alivyopika samaki”.

YES, hata katika maisha yetu, kuna watu kama huyu binti. Iwe makazini, maofisini au popote pale.

Ni watu ambao wanafanya vitu, “As usual” bila kujiuliza, ku-question, au kutazama kwa engo nyingine kwamba kwanini vitu vinafanyika hivyo.

Ukiwauliza kwanini unafanya hivyo atasema;

– Mimi nilipoajiriwa miaka 10 iliyopita nilimkuta Bwana/Bibi fulali akifanya hivi.

– Sisi tumezoea kufanya hivi bana.

– Acha hivyo hivyo.

– Unaweza kuta tangu aingie mahali, hajawahi kubadilisha hata mwonekano au mpangilio wa vitu.

– Vile vile unakuta, wanatumia Formula au approach moja kila siku kufanya jambo fulani.

– Ndiyo wale watu ambao wako tayari kulazimisha njia fulani hata kwa kufoji kwa sababu wamekariri kuwa inafanyika hivyo.

Sasa, jiulize leo, “Je utaendelea kukata samaki katikati hata kama Una chungu kikubwa au utapika mzima mzima?”.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment