Usitazame mazingira aanza.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bila kujali ukubwa wa ndoto uliyonayo, haiwezi kutimia bila kuanza.

Kuna watu ambao wakikuhadithia ukubwa wa ndoto zao, unaweza kujiona wewe si kitu.

Shida yao ni moja tu, wanaongea Ila hawafanyi kabisa.

Mtu anayefanya kidogo kidogo kila siku, atakuja kumzidi ambaye hafanyi kabisa Ila anaongea mambo makubwa.

Mwanafalsafa Socrates, aliwahi kusema kuwa “Let him that would move the world first Move himself”.

Yaani, mtu anayetaka kuubadilisha Ulimwengu, aanze kwanza kufanya kitu yeye mwenyewe.

Usisahau, Umri wako unaenda.

Usisahau kuna watu wanakutana na changamoto Kama ulizonazo Ila wanapambana kila siku.

Ndoto yako haitapata uhai Kama hautaanza kufanya.

Angalia kilicho ndani ya uwezo wako na anza kukifanya leo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment