Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja
Muhtasari
- Marekani Mdukuzi wa Marekani ahukumiwa kwa wizi wa Bitcoin yenye thamani ya mabilioni
- COP 29 Mazungumzo ya COP, ‘hayakidhi malengo’ wataalamu wasema
- Israel na Gaza HRW yaishutumu Israel kwa uhalifu wa kivita huko Gaza
- Ndondi Mike Tyson amzaba kibao mpinzani wake wakati wa upimaji uzani
- Kandanda Mashabiki wapiga filimbi na kuzomea kwenye mechi ya kandanda ya Ufaransa na Israel
- Israel na Syria Israel yashambulia mji wa Damascus wakati Rais Asad wa Syria akikutana na kiongozi wa baraza la ushauri wa Iran
Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Mchana Msomaji Cantona Joseph
Tamasha ‘Amani’ lafutwa mashariki mwa DRC kwa sababu za usalama
Tamasha la “Amani” kwa ajili ya amani huko Goma, ambalo linawaleta pamoja nyota wa kimataifa na viongozi mashuhuri wa muziki wa Kongo mashariki mwa DRC kwa takriban miaka kumi, limefutwa kwa “sababu za kiusalama”, mamlaka imesema.
Toleo la kumi la tamasha hilo ambalo jina lake linamaanisha “amani”, “halitafanyika”, waandaaji wamesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. Tamasha la muziki na dansi, ambalo kwa kawaida huleta pamoja makumi ya maelfu ya watazamaji, lilipaswa kufanyika kuanzia siku ya Alhamisi hadi Jumapili.
Siku ya Jumanne, meya wa Goma alitangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba tamasha hilo “halikuwa limeidhinishwa” kwa “sababu za usalama”. Waandaaji wa tamasha walisikitishwa na uamuzi “wa kusikitisha” na “uliochukuliwa bila taarifa”.
Tukio hilo linachangia “utangamano wa kijamii, ujasiriamali wa vijana” na lina “matokeo makubwa ya kiuchumi kwa jiji la Goma”, wamesema. Wajumbe kadhaa wa kidiplomasia na wasanii wa kigeni tayari walikuwa wamewasili Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, jiji ambalo karibu limezingirwa na M23, waasi wenye silaha unaoungwa mkono na Kigali.
Mwimbaji wa Ufaransa mwenye asil ya Guinea Black M, pamoja na nyota wa rumba wa Kongo kama Ferre Gola walikuwa miongozi mwa nyota ambao wangeshiriki tamasha hilo. Tamasha la “Amani”, lililopangwa kufanyika mwezi Februari, liliahirishwa. Mikutano inayozungumzia dhamira za ikolojia, uwiano wa kijamii na utawala bora pia ilikuwa imepangwa.
Tangu mwisho wa mwaka 2021, mashariki mwa DRC kumekumbwa na kuibuka tena kwa M23, ambayo imeteka maeneo makubwa ya kutoka mikonoi mwa jeshi la Kongo (FARDC) na wanamgambo wenye mafungamano na Kinshasa. Ukiukaji wa makubaliano mapya ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi Agosti yameripotiwa katika wiki za hivi karibuni.
Watu kumi wafariki kwa moto katika nyumba ya uangalizi Hispania

Takribani watu 10 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika moto uliozuka katika nyumba ya uangalizi karibu na Zaragoza kaskazini-mashariki mwa Hispania, huduma za dharura zilisema.
Moto huo ulizuka katika mji wa Villafranca de Ebro mapema Ijumaa asubuhi na maafisa wa eneo hilo walisema watu 82 walikuwa wakiishi katika nyumba hiyo wakati huo.
Kituo hicho kilifunguliwa miaka 16 iliyopita kama nyumba ya Wastaafu, kulingana na ripoti za ndani, lakini tangu wakati huo imekuwa maalumu katika huduma kwa wakazi wenye shida ya afya ya akili.
Huduma za dharura ziliarifiwa mnamo saa 05:00 (04:00 GMT) siku ya Ijumaa na zima moto waliweza kuzima moto huo.
Taarifa zaidi za waliopoteza maisha bado hazijajulikana.
Watu wengine wawili walipelekwa hospitalini, akiwemo mtu mmoja ambaye hali yake ilielezwa kuwa mbaya, meya wa Villafranca de Ebro aliambia redio ya Uhispania.
Volga Ramírez aliiambia Cadena Ser kwamba janga hilo huenda lilisababishwa na godoro lililowaka moto katika moja ya vyumba.
Mdukuzi wa Marekani ahukumiwa kwa wizi wa Bitcoin yenye thamani ya mabilioni

Mdukuzi mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka mitano katika gereza la Marekani kwa kosa la kutakatisha mapato, mojawapo ya wizi mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika sarafu ya kidigitali.
Ilya Lichtenstein alikiri kuwa na hatia mwaka jana katika kesi inayohusisha ubadilishanaji wa fedha wa Bitfinex uliodukuliwa mwaka wa 2016 na wizi wa karibu bitcoin 120,000.
Aliiba pesa hiyo kwa msaada wa mke wake Heather Morgan, ambaye alitumia jina la Razzlekhan kukuza muziki wake wa hip hop.
Wakati wa wizi huo, bitcoin ilikuwa na thamani ya karibu $70m (£55.3m), lakini ilikuwa imepanda thamani hadi zaidi ya $4.5bn wakati walipokamatwa.
Kwa bei za leo zingekuwa na thamani zaidi ya mara mbili ya hiyo.
Mali ya thamani ya $3.6bn iliyorejeshwa katika kesi hiyo ilikuwa mfadhaiko mkubwa zaidi wa kifedha katika historia ya Wizara ya Sheria, Naibu Mwanasheria Mkuu Lisa Monaco alisema wakati huo.
“Ni muhimu kutuma ujumbe kwamba huwezi kufanya uhalifu huu bila kuadhibiwa, kwamba kuna madhara kwao,” hakimu wa wilaya Colleen Kollar-Kotelly alisema.
Lichtenstein, ambaye amekuwa gerezani tangu kukamatwa kwake Februari 2022, alionesha majuto kwa matendo yake.
Pia alisema anatarajia kutumia ujuzi wake kupambana na uhalifu mtandaoni baada ya kumaliza kifungo chake.
Morgan pia alikiri mwaka jana shtaka moja la kula njama ya kutakatisha pesa. Anastahili kuhukumiwa tarehe 18 Novemba.
Kulingana na nyaraka za mahakama, Lichtenstein alitumia zana na mbinu za hali ya juu za udukuzi ili kudukua Bitfinex.
Mazungumzo ya COP ‘hayakidhi malengo’ wataalamu wasema

Mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ya Umoja wa Mataifa COP “hayakidhi malengo” na yanahitaji marekebisho ya haraka, wataalam muhimu akiwemo katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya tabia nchi wamesema.
Katika barua kwa Umoja wa Mataifa, takwimu za juu zinasema nchi hazipaswi kuandaa mazungumzo ikiwa haziungi mkono hatua ya kuondolewa kwa nishati ya mafuta.
Wiki hii rais wa Azerbaijan aliwaambia viongozi wa dunia waliokusanyika nchini mwake kwa ajili ya COP29 kwamba gesi asilia ni “zawadi kutoka kwa Mungu” na hapaswi kulaumiwa kwa kuileta sokoni.
Hayo yanajiri siku chache baada ya BBC kuripoti kwamba afisa mkuu wa Azerbaijan alionekana kutumia nafasi yake katika COP kupanga mkutano kujadili uwezekano wa mikataba ya nishati ya kisukuku.
Mazungumzo hayo yamepata maendeleo makubwa katika miaka ya hivi karibuni, licha ya ukweli kwamba makubaliano ya pamoja yanahitajika kati ya karibu nchi 200 kuchukua hatua.
Mkataba wa hali ya hewa wa Paris, uliotiwa saini mwaka wa 2015, unaeleza mpango wa muda mrefu wa kudhibiti ongezeko la joto, huku nchi zikijitahidi kuweka ongezeko hilo chini ya 1.5C karne hii.
Pia wamekubali kuhama kutoka kwenye nishati ya mafuta katika mifumo ya nishati, na kuongeza nishati mbadala ifikapo 2030.
Lakini wakati waandishi wa barua hii wanatambua mafanikio haya, wanahisi kuwa mchakato wa COP unaosonga polepole “haufai tena kutimiza kusudi lao” katika kukabiliana na changamoto ya tabia nchi inayokwenda kwa kasi.
“Muundo wake wa sasa hauwezi kuleta mabadiliko kwa kasi na kiwango kikubwa, ambayo ni muhimu kuhakikisha hali ya hewa inafika kwa usalama kwa wanadamu,” watia saini wake walisema.
Miongoni mwao ni Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon, mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya hali ya hewa Christiana Figueres na rais wa zamani wa Ireland Mary Robinson.
HRW yaishutumu Israel kwa uhalifu wa kivita huko Gaza

Israel imefanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kusababisha kwa makusudi wakimbizi wengi wa Wapalestina huko Gaza, ripoti ya Human Rights Watch (HRW) inasema.
Takribani watu milioni 1.9, 90% ya wakazi wa Gaza, wamekimbia makazi yao katika kipindi cha mwaka uliopita, na 79% ya eneo hilo liko chini ya maagizo yaliyotolewa na Israeli, kulingana na UN.
Ripoti ya HRW inasema hii ni sawa na “uhamisho wa lazima” na kwamba “ushahidi unaonesha kuwa umekuwa wa utaratibu na sehemu ya sera ya serikali”.
Pia inasema vitendo vya Israeli vinaonekana “kukidhi utakaso wa kikabila”. Israel ilisema ripoti hiyo “ni ya uwongo kabisa na imejitenga na ukweli”.
“Kinyume na madai katika ripoti ya HRW, juhudi za Israel zinaelekezwa tu katika kusambaratisha uwezo wa ugaidi wa Hamas na sio kwa watu wa Gaza,” Oren Marmorstein, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel alichapisha kwenye X.
Aliongeza kuwa Israel “itaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ya migogoro ya silaha”.
HRW pia imeshutumu Hamas kwa kutumia raia kama ngao za binadamu kwa kufanya kazi ndani ya nyumba na miundombinu ya kiraia.
Israel yashambulia mji wa Damascus wakati Rais Asad wa Syria akikutana na kiongozi wa baraza la ushauri wa Iran

Shirika la habari la serikali ya Syria linasema kuwa takribani watu 15 waliuawa wakati wa mashambulizi ya anga ya Israel kwenye majengo mawili ya makazi magharibi mwa Damascus.
Kwa mujibu wa ripoti hii, moja ya majengo hayo yapo katika kitongoji cha Meze mjini Damascus, ambayo ni makao makuu ya taasisi za usalama, balozi na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jengo la pili liko katika kitongoji cha Qudsiya magharibi mwa Damascus.
Wakati huo huo, Reuters iliandika kwamba Israeli, wakati ikithibitisha mashambulio hayo, ilisema kwamba “maeneo ya jeshi” pamoja na makao makuu ya Islamic Jihad lilipigwa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, afisa wa kundi la Palestina Islamic Jihad nchini Syria, ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameliambia shirika hili la habari kwamba moja ya ofisi zake ililengwa katika shambulio la kitongoji cha Meze na wanachama kadhaa wa kundi hilo waliuawa.
Shambulio hili lilitekelezwa wakati wa uwepo wa Ali Larijani, mshauri wa kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria, na mikutano yake na Bashar Assad na maafisa wengine wa Syria. Haijulikani kuwa Bwana Larijani alikuwa bado Damascus na Syria wakati wa shambulio hili.
Mike Tyson amzaba kibao mpinzani wake wakati wa upimaji uzani

Mike Tyson alimpiga makofi Jake Paul wakati wa kupima uzito kwa ajili ya pambano la siku ya Ijumaa la uzito wa juu huko Texas.
Bondia mchanga, Paul, 27, atamenyana na Tyson mwenye umri wa miaka 58 kwenye Uwanja wa AT&T mjini Dallas.
Baada ya wote wawili kupimwa uzito , paul alitambaa katika sakafu kabla ya kuinuka na kusimama mbele ya Tyson wakati wawili hao walipokutanishwa
Tyson alikuwa amekataa kujihusisha na Paul kwa muda mrefu wa wiki ya mapigano, lakini alimpiga mpinzani wake usoni, na kusababisha maafisa wa usalama na wafuasi kukimbilia kuwatenganisha wapiganaji.
“Mazungumzo yamekwisha,” Tyson alisema na kuondoka kwenye jukwaa. Wakati huo huo, Paul alikuwa akitabasamu kabla ya kukaa chini na kuonekana kutafakari.
“Hata sikuhisi. Ana hasira. Yeye mwenye hasira,” Paul alilizungumzia kofi.
“Mike Tyson, nilidhani kwamba ni kofi la kawaida, rafiki, lakini kesho utapigwa.”
Bingwa wa dunia mara mbili Tyson mara ya mwisho alipanda ulingoni mwaka 2005.
Mashabiki wapiga filimbi na kuzomea kwenye mechi ya kandanda ya Ufaransa na Israel

Baadhi ya mashabiki wa soka waliohudhuria mechi ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya mjini Paris kati ya Ufaransa na Israel walipiga filimbi na kuzomea wakati wimbo wa taifa wa Israel ukipigwa mwanzoni mwa mchezo huo.
Mechi ya Alhamisi ilichezwa mbele ya umati mdogo wa watu na ulinzi mkali wiki moja baada ya vurugu huko Amsterdam kati ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina na mashabiki wa Israeli waliozuru huko.
Licha ya hofu ya kujirudia kwa vurugu za Amsterdam, kulikuwa na mikwaruzano machache tu kwenye viwanja wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo, ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0.
Rais Emmanuel Macron, ambaye alihudhuria mechi hiyo na Waziri Mkuu Michel Barnier , alisema kabla kwamba Ufaransa haitakubali chuki dhidi ya Wayahudi.
Maelfu ya polisi walitumwa kuhakikisha usalama unakuwepo katika uwanja wa Stade de France kaskazini mwa vitongoji vya Paris na kwenye usafiri wa umma, huku kitengo cha polisi cha kupambana na ugaidi kikilinda kikosi cha Israel.
Ripota wa shirika la habari la AFP la Ufaransa alishuhudia wasimamizi wakiingilia kati ili kukomesha makabiliano kati ya mashabiki pinzani.
Kulingana na shirika la habari la Reuters, baadhi ya mashabiki kati ya 100 wa Israel walikaidi maonyo ya usafiri kutoka kwa serikali yao na kuketi kwenye kona ya uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000.
Wakipunga maputo ya manjano, waliimba “Waachilie Mateka” wakirejelea Waisraeli wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, shirika hilo linaripoti.
Kabla ya mechi hiyo, waandamanaji mia kadhaa walikusanyika karibu na uwanja huo kupeperusha bendera za Palestina, Lebanon na Algeria kupinga vita huko Gaza.
Mahakama ya Afrika yaipa Kenya miezi 3 kutekeleza amri kuhusu jamii ya Ogiek
Amri hiyo ilitolewa na AfCHPR siku ya Novemba 12, jijini Arusha, Tanzania.

Jamii ya Ogiek ambao ni wawindaji kiasili, inakadiriwa kuwa ni jumla ya watu 45,000m huku wakitegemea zaidi msitu wa Mau nchini Kenya kama uhai wao. @OgiekPeoples
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imeipa serikali ya Kenya miezi mitatu kuipa mahakama hiyo mrejesho wa utekelezwaji wa maamuzi ya keshi namba 006/2012 iliyotolewa na hiyo inayoketi jijini Arusha, nchini Tanzania.
Mahakama hiyo, pia iliitaka Kenya kutengeneza sera maalumu za kuilinda jamii asili ya Ogiek nchini humo.
Mwezi Mei mwaka 2022, Mahakama ya AfCHPR ilibaini kuwa serikali ya Kenya ilikiuka haki ya kuishi, kumiliki mali, maliasili, maendeleo, dini na utamaduni wa jamii ya Ogiek, kwa mujibu wa Katiba ya Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu.

Kwa upande wake, serikali ya Kenya iliomba kuahirishwa kwa usikilizwaji wa shauri hilo, ili iweze kuwasilisha baadhi ya hatua za utekelezwaji wa hukumu hiyo.
Jamii ya Ogiek, ambao ni wawindaji kiasili, inakadiriwa kuwa ni jumla ya watu 45,000m huku wakitegemea zaidi msitu wa Mau nchini Kenya kama sehemu ya uhai wao.
Hata hivyo, jamii hiyo imekuwa ikiondolewa nje ya msitu huo na maofisa uhifadhi KFS na KWS.
SAMIA ANATARAJIA KUFANYA ZIARA NCHINI BRAZIL G20
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Brazil ambapo pia atashiriki mkutano wa Wakuu waNchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa kundi la G20 utakaofanyika Novemba 18 hadi 19,2024 Jijini Rio de Janeiro.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa Rais Samia amealikwa na Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil na Mwenyekiti wa G20 kushiriki mkutano huo wenye lengo la kukuza ushirikiano wa kimataifa kwenye masuala yakiuchumi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki mkutano wa G.20, na mwaliko huo unatokana na heshima na ushawishi ambao Rais Samia amejijengea kwenye majukwaa ya kimataifa.
Pamoja na mambo mengine katika mkutano huo Rais Samiaanatarajiwa kushiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umasikini kuchochea maendeleo endelevu na matumizi ya nishati mbadala.
Rais Samia anatarajiwa kutumia jukwaa hilo linalokutanisha nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani kuelezea jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha kuna usalama wa chakula,kupunguza umaskini, kujenga maendeleo endelevu na kutafuta fursa za ushirikiano zitakazowaletea ustawi Watanzania kupitia sekta za uzalishaji.
Akiwa nchini Brazil, Rais Samia atafanya mikutano yapembezoni na taasisi kubwa za kifedha duniani pamoja na kukutana kwa mazungumzo na Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na baadhi ya nchi wanachama wa G.20 akiwemo mwenyeji wake Rais wa Brazil.
WAKATI HUOHUO
Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wasanii na wapenzi wote wa muziki nchini kufuatia kifo cha mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram, Rais Samia ameandika
“Kwa zaidi ya miaka 50 King Kikii ametoa burudani kwa mamilioni ya Watanzania, na amekuwa mlezi na mwalimu wa wengi katika tasnia ya muziki. Tutamkumbuka na kumuenzi kwa kazi zake nyingi na nzuri ikiwemo wimbo wake maarufu wa ‘Kitambaa Cheupe’ ambao umeendelea kuwa sehemu ya burudani kwenye maeneo na shughuli mbalimbali za burudani nchini”.
King Kikii amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 15, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
KIPENGA CHA MICHEZO–TETESI ZA SOKA ULAYA
Timu ya taifa ya Uganda yafuzu AFCON 2025

Uganda inakuwa timu ya pili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kufuzu michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada ya DRC, huku Tanzania ikisubiri kujua hatma yake siku ya Novemba 16, 2024, itakapovaana na Ethiopia./Picha: Wengine
Timu ya Taifa ya Uganda, maarufu kama ‘The Uganda Cranes’ imefuzu kushiriki ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), ikiwa imebakiza mechi mbili kibindoni.
‘The Uganda Cranes’ ilijihakikishia tiketi ya AFCON 2025 baada ya Sudan Kusini kuifunga Congo kwa mabao 3-2 jijini Juba, siku ya Alhamisi.
Matokeo hayo, yanaifanya Congo kubakia katika nafasi ya tatu, ikiwa imejikusanyia alama 4, ikiwa haina uwezo wa kuzipiku Uganda na Afrika Kusini zenye alama 10 na 8 mtawalia.
Uganda inakuwa timu ya pili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kufuzu michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada ya DRC, huku Tanzania ikisubiri kujua hatma yake siku ya Novemba 16, 2024, itakapovaana na Ethiopia.
Hii inakuwa mara ya nane kwa Uganda kushiriki michuano ya AFCON, ikiwa imeshashiriki mwaka 1962, 1974, 1976, 1978, 2017 na 2019.
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 15.11.2024

Beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold anaendelea kukataa ofa za kuongeza mkataba wake Anfield huku Real Madrid wakiendelea na mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mkataba wake wa sasa utakapokamilika msimu ujao wa joto. (Relevo – Spanish)
West Ham wanatarajiwa kusimama kidete kumuuza kiungo mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus kwa pauni milioni 85 huku Arsenal na Liverpool zikimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail – Subscription Required)
Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso ataondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga mwishoni mwa msimu huu licha ya kusaini kandarasi hadi 2026, huku Real Madrid ikitarajiwa kuwa eneo analotarajiwa kuelekea. (Eurosport In Spanish)

Barcelona wanavutiwa na beki wa kushoto wa Wolves Mhispania Hugo Bueno, 22, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Feyenoord ya Uholanzi. (Sport – In Spanish)
Real Madrid wamefanya uchunguzi wa kwanza kutaka kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Ujerumani wa Bayer Leverkusen Jonathan Tah. Barcelona, Bayern Munich na vilabu vya Premier League vinadaiwa kumfuatilia beki huyo ambaye mkataba wake na Leverkusen unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (AS – In Spanish)
Nottingham Forest haina shinikizo la kumuuza beki wa kati wa Brazil Murillo mwenye umri wa miaka 22 mwezi Januari baada ya kutakiwa na Real Madrid. Beki huyo ana thamani ya £40m. (Daily Mail, )
Manchester United na Liverpool wanamfuatilia beki wa kushoto wa Fulham Antonee Robinson, 27, baada ya kuanza vyema msimu huu. Klabu hiyo ya London inasemekana kusita kumruhusu Mmarekani huyo kuondoka wakati wa msimu huu, ikiondoa uwezekano wa kuhama Januari. (Football Insider,)

Liverpool na Chelsea ni miongoni mwa vilabu vilivyotuma maskauti kumtazama kiungo wa kati Andrija Maksimovic mwenye umri wa miaka 17 ingawa wameambiwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia hataondoka Red Star Belgrade kwa bei nafuu. (TeamTalks)
Barcelona wamepanga orodha fupi ya wachezaji inaowalenga mwezi wa Januari akiwemo winga wa Napoli kutoka Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23 na fowadi wa AC Milan wa Ureno Rafael Leao, 25. (Diario Sport – In Spanish).
Crystal Palace wamewasiliana na Chelsea kuhusu kumsajili winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk, 23, kwa mkopo mwezi Januari. (Football Transfers)
Liverpool haitaraji kumtoa fowadi wa Italia Federico Chiesa, 27, licha ya ripoti za kurejea Serie A. (The Athletic – Subscription Required)

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayer Leverkusen Simon Rolfes yuko kwenye rada za Arsenal kuchukua nafasi ya Edu kama mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo. (Barua – Subscription Required)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 31, ataondoka rasmi Juventus siku chache zijazo na kuwa mchezaji huru. (Gazzetta dello Sport – In Itali)
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.