Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International katika ripoti yake, inaonesha kuwa vifaa vya kijeshi vilivyotengezwa nchini Ufaransa, vinatumiwa kwenye vita vinavyoendelea nchini Sudan.
Silaha hizo, yakiwemo magari ya kijeshi, zimekuwa zikisafirishwa nchini Sudan na nchi ya Falme wa Kiarabu, kinyume na azimio la Umoja wa Mataifa linalozuia ungizwaji wa silaha nchini humo hasa katika jimbo la Sudan tangu mwaka 2004.
Amnesty Internatonal inasema vifaa hivyo vya kijeshi vilivyotengezwa na kampuni za Ufaransa KNDS na Lacroix vinaonekana kwenye uwanja wa vita katika mapambano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

Katibu Mkuu wa Amnesty International Agnes Callamard amesema, utafiti wao umeonesha kuwa, silaha hizo za Ufaransa zinaendelea kutumiwa, yakiwemo magari ya kisasa yanayotumiwa kwenye uwanja wa vita.
Shirika hilo linataka kukomeshwa uingizwaji wa silaha hizo nchini Sudan kutoka kwa nchi ya Falme za Kiarabu na Ufaransa kutumia ushawishi wake, kuizuia nchi hiyo ya Mashariki ya Kati kuacha kukiuka zuio la kuingizwa kwa silaha hizo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.