Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mwanasiasa wa Mali Issa Kaou N’Djim, amekamatwa na kuzuiwa jijini Bamako, baada ya kushtumiwa kutoa matamshi ya chuki dhidi ya uongozi wa nchi jirani ya Burkina Faso ambayo pia inaongozwa na jeshi.
Mwanasiasa maarufu huyo ambaye aliwahi kuhudumu katika serikali ya mpito na kuumuunga mkono kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita na baadaye kutofautiana naye, alikamatwa siku ya Jumatano kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi dhidi ya uongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso, wakati akihojiwa na Televisheni binafsi, Joliba TV.
Mamlaka ya kudhibiti vyombo vya Habari nchini Burkina Faso imesema matamshi ya mwanasiasa huyo kuwa kulikuwa na jaribio la la mapinduzi katika nchi hiyo yalilenga kutikisa uongozi wa kijeshi na kuwachochea wananchi wa Burkina Faso.

Tangu alipojitenga na uongozi wa kijeshi na kushinikiza uongozi wa nchi tahe kurejea kwa raia, N’Djim amewahi kukamatwa mwaka 2021 na kuhukumiwa kifungo kilicholeweshwa cha miezi sita jema kwa kuchapisha maandishi ya kuukoa uongozi wa kijeshi.
Jitihada zake wa kuondoka nchini Mali, zimegonga mwamba mara kadhaa na sasa anakabiliwa na kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi dhidi ya Burkina Faso ambayo mara kwa mara imewakamata wakosoaji wa serikali ya kijeshi, wakiwemo wanasiasa, wanaharakati na wanahabari.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.